TRA

TRA

Tuesday, June 13, 2017

Wachimbaji wafukiwa, Mkuu wa wilaya atoa maagizo

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela akizungumza na blog hii juu ya kitu kinachiendelea kwenye mgodi wa nyakavangala.

Na Fredy Mgunda, Iringa

Wachimbaji wa madini katika mgodi wa nyakavangala wamefukiwa na mchanga kutokana na wachimbaji hao kuingia kinyume cha makubaliano yaliyowekwa baina ya wachimbaji na Mkuu wa Wilaya ya Iringa  Richard Kasesela.

Akizungumza na blog hii, Kasesela alisema kuwa jana kuwa duara la mgodi mmoja ulioko Nyakavangala uliporomoka na kufukia wachimbaji wanne. 

"Inasemekana wachimbaji hao walikuwa wameingia kuiba kwani duara hilo ni kati ya maduara ambayo Mkuu Wa wilaya ya Iringa  Mhe Richard Kasesela aliifungia ili ijengwe nguzo na ngao" alisema Kasesela

Kasesela alisema kuwa watu 4 waliingia mgodini baada ya mafundi  Wa ujenzi Wa ngao kupumzika kwa vile ni usiku ndipo wachimbaji nao wakaingia mgodini bila ruhusa.

"Hadi sasa tumefanikiwa kuokoa 3 hadi sasa huyo mmoja hajaokolewa bado yupo ndani ya mgodi kutokana na changamoto za uokoaji ili Juhudi zinaendelea za kumuokoa huyo mmoja" alisema Kasesela

Kasesela alisema kuwa changamoto ilikuwa ni namna ya kumuokoa kwani sehemu iliyokuwa imejifukia juu mwamba mwingine ulionekana kuwa na dalili za kushuka.ikawapasa kujengea kwanza eneo hilo kazi iliyochukua mda mrefu na ndipo waaze kuokoa.kwahiyo tunasubiri hatua nyingine sasa.

"Naendelea kuwaonya wachimbaji wasiendelee na uchimbaji eneo la chini maarufu kama kwenye "vein" mpaka wajenge ngao ili wasihatarishe maisha yao. Wakiendelea na kiburi tutaamua tufunge mgodi" alisema Kasesela

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger