MKUU wa Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga, Mhandisi
Robert
Gabriel akizungumza wakati makabidhiano ya vyumba vya madarasa vitano
na vyoo ishirini na nne,mradi maji na uzio wa shule ya msingi jitengeni
iliyopo Mji mdogo wa Mombo uliofanywa na taasisi isiyo ya kisherikali A
better World ya Canada ikishirikiana na Vuga development Initiative
kulia ni Founder wa A Better World Canada Eric Rajabu na Mkurugenzi wa
Taasisi ya A Better Worild Canada
nchini Tanzania,Aizidi Kaoneka
Founder
wa A Better World Canada Eric Rajabu kushoto akizungumza katika halfa
hiyo kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya A Better Worild Canada nchini
Tanzania,Aizidi Kaoneka
Mkurugenzi wa Taasisi ya A Better Worild Canada nchini Tanzania,Aizidi Kaoneka akizungumza katika halfa hiyo
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Korogwe Vijijini,Gorge Nyaronga akizungumza katika halfa hiyo
MKUU wa wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga,Mhandisi Robert Gabriel kushoto akimpatia zawadi ya kitenge Founder wa A Better World Canada Eric Rajabu akimshukuru kwa msaada wa ujenzi wa madarasa na vyoo na uzio
Founder wa A Better World Canada Eric Rajabu katikati akitazama kitenge chake
Risala ya shule hiyo ikisomwa
Sehemu ya vyumba vya madarasa vilivyojengwa
Wanafunzi wa shule ya Msingi Jitengeni wilayani Korogwe wakitumbuiza wakati wa hafla hiyo
MKUU
wa wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga,Mhandisi Robert Gabriel akizungumza
wakati makabidhiano ya vyumba vya madarasa vitano na vyoo ishirini na
nne,mradi maji na uzio wa shule ya msingi jitengeni iliyopo Mji mdogo wa
Mombo uliofanywa na taasisi isiyo ya kisherikali A better World ya
Canada ikishirikiana na Vuga development Initiative
SERIKALI
wilayani Korogwe Mkoani Tanga imepania kuhakikisha wanakomesha vitendo
vya mimba za utotoni kwa kuwachukulia hatua kali watakaobinika kuhusika
na matukio hayo ili kuweza kuondosha hali hiyo kwenye jamii.
Lakini
pia imesema watakaohusika kuwa kichocheo cha ndoa hizo zifanyike
wakiwemo wazazi kutoka pande zote mbili watafikishwa mahakamani ili
sheria zichukue mkondo wake zaidi kwa lengo la kukomesha vitendo vya
namna hiyo kwenye jamii.
Hayo
yalibainishwa na Mkuu wa wilaya ya Korogwe ,Mhandisi,Robert Gabriel
wakati makabidhiano ya vyumba vya madarasa vitano na vyoo ishirini na
nne,mradi maji na uzio wa shule ya msingi jitengeni iliyopo Mji mdogo wa
Mombo uliofanywa na taasisi isiyo ya kiserikali A better World ya
Canada ikishirikiana na Vuga development Initiative
.
Alisema
hatua hiyo ina lengo la kuhakikisha wanakomesha vitendo vinavyofanya na
baadhi ya vijana vya kuwa sha wishi wananfunzi wa kike na kuwapatia
ujauzito hivyo kupelekea wasichana hao kukatisha masomo yao.
Mkuu
huyo wa wilaya alisema hivi sasa lazima wawe wakali na watu wanaocheza
na maisha ya watoto ya wanafunzi ambao asilimia kubwa masomo yao yana
haribiwa mara tu baada ya kushawishiwa na kupewa ujauzito.
Alisema
hatua ya kurubuniwa watoto wa kike kwenye masomo haiwezi kuvumiliwa
hasa kipindi hiki ambacho hawatakuwa na nafasi tena ya kujiendeleza
katika shule za serikali pindi watakapo jifungua.
Awali
akizungumza wakati wa hafla hiyo ,Mkuu wa shuele ya msingi
Jitengeni,Mafikiri Twinzi alisema umalizikaji wa madarasa hayo
utapunguza kero kwa wanafunzi shuleni hapo ambapo awali walikuwa wakikaa
wanafunzi 100 hadi 120 kwenye chumba kimoja.
Alisema shule hiyo iliyo na wanafunzi 816 imekuwa na tatizo la
uchakavu wa madarasa hali iliyopelekea kuwajengea woga wanafunzi wa kuangukiwa na kuta za shule hiyo.
Naye
kwa upande wake,Mkurugenzi wa Taasisi ya A Better Worild Canada nchini
Tanzania,Aizidi Kaoneka alisema taasisi hiyo lengo lake ni kuisadiana na
serikali katika kuboresha huduma za kijamii ikiwemo elimu,afya na maji.
Aidha
alisema baada ya kumalizika kwa ujenzi wa madarasa hayo,matundu ya
vyoo,uzio pamoja na kuweka mabomba ya maji na sasa mpango uliopo ni
kuendelea kuvunja madara manne mengine yaliyochakaa shuleni hapo ili
kujenga upya na kutoa fursa kwa wanafunzi kujisomea bila kuwepo kwa
vikwazo vya aina yeyote ile.
Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha
SHARE
No comments:
Post a Comment