Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB,
Bw. Francis Assenga (kushoto) akisisitiza nafasi ya Benki yake katika
kuleta matokeo makubwa kwenye mapinduzi ya kilimo na viwanda hasa vya
uchakakataji na usindikaji wa mazao ya kilimo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi
ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB), Bibi Rosebud
Kurwijila (kushoto) akizungumza na aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Wizara
ya Kilimo, Mzee Peniel Lyimo (kulia) wakati wa Kikao cha Wadau wa Kilimo
Kujadili Mikakati Ya Kuboresha Uwezeshaji Kwenye Kilimo Na Viwanda
kinachofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere
(JNICC) Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya Biashara
ya TADB, Bibi Rehema Twalib (kulia) akizungumza wakati wa Kikao cha
Wadau wa Kilimo Kujadili Mikakati Ya Kuboresha Uwezeshaji Kwenye Kilimo
Na Viwanda kinachofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa
Julius Nyerere (JNICC) Dar es Salaam.
Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mzee Peniel Lyimo (kulia) akiongoza Kikao hicho.
Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa
TADB wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi, Bibi Rosebud Kurwijila (kushoto)
wakifuatilia kwa makini Kikao hicho.
Washiriki wa Kikao hicho
wakifuatilia mawasilisho mbali mbali wakati wa Kikao cha wadau wa kilimo
waliokutana kujadili mikakati ya kuboresha uwezeshaji kwenye kilimo na
viwanda. Kikao hicho kiliandaliwa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya
Tanzania (TADB).
Wadau wa kilimo waliokutana kujadili mikakati ya kuboresha uwezeshaji kwenye kilimo na viwanda wakiwa katika picha ya pamoja.
…………………..
Na Mwandishi wetu,
Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya
Tanzania (TADB) imekutana na wadau wa kilimo ili kujadili mikakati ya
kuboresha uwezeshaji kwenye kilimo na viwanda katika kuhakikisha Benki
hiyo inasaidia sekta ya Kilimo iweze kusukuma dhamira ya Serikali ya
kujenga Uchumi wa Viwanda.
Akizungumza katika kikao hicho
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga amesema kuwa
Benki imejipanga kuleta matokeo makubwa kwenye mapinduzi ya kilimo na
viwanda hasa vya uchakakataji na usindikaji wa mazao ya kilimo.
Bw. Assenga amesema kuwa mipango
hii itasaidia upatikanaji wa mali ghafi kwa viwanda vya ndani hivyo
kusukuma ndoto ya Serikali kufikia lengo lake la Kujenga Uchumi wa
Viwanda na kuhuisha uwekezaji kwenye Viwanda vidogo vidogo na vya kati
vya usindikaji na uchakataji wa mazao ya Kilimo na mifugo.
“Benki imejikita kwenye kusaidia
Sekta ya Kilimo iweze kusukuma dhamira ya Serikali ya Uchumi wa Viwanda
uweze kutoa matunda yaliyokusudiwa ili kuchagiza na kusaidia Mapinduzi
ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia
kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini,” alisema.
Bw. Assenga amesema katika
kuhakikisha azma hiyo inatimia TADB imejipanga kutoa elimu ili
kuwajengea uwezowakulima na taasisi mbali mbali za fedha pamoja na vyama
vya ushirika kuweza kukopa toka TADB pamoja na kushirikiana na wadau
mbali mbali kusaidia uwekezaji mkubwa kwenye Sekta ya Kilimo ili iweze
kuinua pato la Taifa na kumkomboa Mwananchi.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji huyo
ameongeza kuwa TADB imeanza kujiimarisha na kuchochea mabenki na
taasisisi za fedha kuongeza utoaji wa mikopo na fedha zingine kwenye
Sekta ya Kilimo ili kuongoza utoaji mikopo ya uongezaji wa thamani
katika shughuli za kilimo.
TADB ni taasisi ya serikali ambayo
ilianzishwa kwa ajili ya kutatua ufinyu mkubwa wa upatikanaji wa fedha
mikopo kwa ajili ya maendeleo ya kilimo nchini ambao ulikuwa unachangiwa
kwa kiasi kikubwa na mikopo mingi kutoka taasisi za fedha kuelekezwa
zaidi kwenye upande wa biashara za bidhaa; riba kubwa kwenye mikopo ya
kilimo; mikopo ya muda mfupi; masharti magumu ya kukopa bila kuzingatia
hali halisi ya sekta ya kilimo na mazao ambayo inaathiriwa kwa kiasi
kikubwa na mabadiliko ya hali ya hewa.
SHARE
No comments:
Post a Comment