• About
  • Services
  • Products
  • Blog
  • Contact Us

NCHI YANGU

Menu
  • Home
  • Lifestyle
    • Sub Menu 1
    • Sub Menu 2
    • Sub Menu 3
  • Sports
    • Sub Menu 1
      • Sub Menu 1
      • Sub Menu 2
      • Sub Menu 3
    • Sub Menu 2
    • Sub Menu 3
  • Post
  • Fitness
  • Music
  • Travel
  • Politics
  • Beauty

TRA

TRA

Saturday, June 3, 2017

Home > > UEFA: Bingwa kati ya Juventus v Real Madrid kufahamika leo

UEFA: Bingwa kati ya Juventus v Real Madrid kufahamika leo

at 4:02 AM
Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !
Mkufunzi mkuu wa Real Madrid Zinedine Zidane anakabiliwa na kizungumkuti cha kuamua nani kati ya Gareth Bale na Isco atacheza katika fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya leo.

Bale hajacheza tangu 23 Aprili lakini sasa yuko sawa kucheza.
Isco, ambaye alijaza pengo lake naye amekuwa akicheza vyema sana na amefunga mabao matano katika mechi nane walizocheza hivi karibuni.

"Wote wawili ni wachezaji muhimu sana na kila mmoja anaweza kutoa maoni yake lakini hilo halitaniathiri," Zidane amesema.
Mkufunzi wa Juventus Max Allegri wachezaji wake wote pia wako sawa kucheza.

Gianluigi Buffon, Giorgio Chellini, Alex Sandro, Mario Mandzukic na Leonardo Bonucci walipumzishwa mechi ya mwisho ya Juve katika Serie A dhidi ya Bologna Jumamosi iliyopita.

Gianluigi Buffon, 39, atakuwa nahodha wa Juve katika mechi hiyo itakayochezewa Cardiff.
  • Borussia Dortmund na Legia Warsaw wavunja rekodi
Buffon hajawahi kushinda Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
"Itakuwa na maana kubwa sana kwangu," anasema mchezaji huyo, ambaye amechezea Italia mechi 168.

 Bale na Isco wakitaniana wakati wa mazoezi, mmoja wao huenda atakosa nafasi ya kucheza

"Itakuwa siku ya furaha zaidi kwangu katika maisha yangu ya uchezaji, pamoja na Kombe la Dunia - kwa sababu itakuwa ni kama zawadi, baada ya safari ngumu yenye dhiki na visiki na bidii."
Juventus walilaza Monaco 4-1 na kufika fainali kwa mara ya pili katika misimu mitatu.
Real Madrid nao waliwatoa Atletico kwa ushindi wa jumla wa 4-2.
Ronaldo, ambaye alifunga penalti ya ushindi fainali msimu uliopita, anasema amepumzika vya kutosha na ako makini kabisa.
"Mwisho wa msimu ni muhimu sana," anasema.
Ronaldo alifikia magoli 400 ambayo amefungia Real msimu wa sasa, pamoja na mabao 100 Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Haki miliki ya picha PA
Image caption Usalama utaimarishwa kwa ajili ya fainali
Hii itakuwa mechi ya 19 kwa klabu hizo mbili kukutana, mechi zote zikiwa katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya/Kombe la Ulaya.
Klabu hizo ndizo zilizokutana mara nyingi kabisa historia ya michuano hiyo, baada ya Bayern dhidi ya Real Madrid (24).
Juventus na Real Madrid, kila mmoja ameshinda mechi nane kati ya hizo, mechi mbili zikimalizika kwa sare.
Mechi yao pekee kukutana fainali Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, Real walishinda 1-0 mwaka 1998 kupitia bao la Pedrag Mijatovic.
Juventus wameshinda mara mbili pekee kati ya fainali nane walizocheza Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya/Kombe la Ulaya. Walishindwa fainali nne walizocheza karibuni zaidi mwaka 1997, 1998, 2003 na 2015.
Real Madrid wanapigania kuwa klabu ya kwanza tangu AC Milan (1989, 1990) kushinda Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya/Kombe la Ulaya misimu miwili mfululizo.
Mwaka huu ni mara ya tatu kwa Real Madrid kufika fainali katika misimu minne.
Juve ndiyo klabu pekee ambayo haijashindwa mechi yoyote msimu huu Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, klabu ya kwanza tangu Atletico Madrid mwaka 2013/14 kufika fainali bila kushindwa.
Real Madrid nao wamefunga kila mechi kati ya mechi 12 walizocheza Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu huu.
Unknown

Author: Unknown

SHARE
  • Share
  • Tweet
  • Share
  • Pin
  • Share
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post
Fourni par Blogger CodeEnvoyer par emailBlogThis !Partager sur TwitterPartager sur FacebookPartager sur LinkedInÉpingler sur PinterestPartager sur StumbleUponVoter pour cet article sur HelloCoton

No comments:

Post a Comment

Newer Post Older Post Home
Subscribe to: Post Comments (Atom)

Tupate kupitia Facebook

Popular Posts

  • JE, UNAFAHAMU HISTORIA YA MUADHAMA ASKOFU MKUU POLYCARP KARDINALI PENGO? SOMA HAPA
      Muadhama Askofu Mkuu Polycarp Kardinali Pengo wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam akipongezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya...
  • ANGALIA HAPA. WATUMISHI WA WIZARA YA MAMBO YA NJE WAHITIMU MAFUNZO YA JKT
    Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa wamejipanga kusubiri sherehe za mahafali ya kum...
  • Wakurugenzi watatu wajiuzulu kupinga ubaguzi
    Wakurugenzi watatu wa juu wamejiuzulu kutoka katika baraza la uchumi na uzalishaji la Ikulu ya Marekani, wakati rais Donald Trump aki...

Popular Posts

  • JE, UNAFAHAMU HISTORIA YA MUADHAMA ASKOFU MKUU POLYCARP KARDINALI PENGO? SOMA HAPA
    JE, UNAFAHAMU HISTORIA YA MUADHAMA ASKOFU MKUU POLYCARP KARDINALI PENGO? SOMA HAPA
      Muadhama Askofu Mkuu Polycarp Kardinali Pengo wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam akipongezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya...
  • ANGALIA HAPA. WATUMISHI WA WIZARA YA MAMBO YA NJE WAHITIMU MAFUNZO YA JKT
    ANGALIA HAPA. WATUMISHI WA WIZARA YA MAMBO YA NJE WAHITIMU MAFUNZO YA JKT
    Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa wamejipanga kusubiri sherehe za mahafali ya kum...
  • Wakurugenzi watatu wajiuzulu kupinga ubaguzi
    Wakurugenzi watatu wa juu wamejiuzulu kutoka katika baraza la uchumi na uzalishaji la Ikulu ya Marekani, wakati rais Donald Trump aki...
  • WAZIRI UMMY AENDESHA MKUTANO WA BARAZA LA KISEKTA LA MAWAZIRI WA AFYA WA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI
    WAZIRI UMMY AENDESHA MKUTANO WA BARAZA LA KISEKTA LA MAWAZIRI WA AFYA WA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI
    M...
  • RAIS DKT. MAGUFULI AZUNGUMZA NA MAAFISA WA JESHI LA POLISI WALIOPANDISHWA VYEO IKULU JIJINI DAR ES SALAAM,AWATAKA KUCHUKUA HATUA DHIDI YA WANAOLETA MATATIZO
    RAIS DKT. MAGUFULI AZUNGUMZA NA MAAFISA WA JESHI LA POLISI WALIOPANDISHWA VYEO IKULU JIJINI DAR ES SALAAM,AWATAKA KUCHUKUA HATUA DHIDI YA WANAOLETA MATATIZO
    Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Ahmada Abdalla Khamis akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe...
  • Ufaransa: Waziri mkuu wa zamani Francois Fillon aongoza mbio za Urais
      Mojawapo ya vipaumbe...

Pages

  • Home
  • About Us
  • Contat Us
 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger