TRA

TRA

Tuesday, June 13, 2017

VETA na Airtel watangaza kozi 5 mpya za ufundi stadi kupitia simu ya mkononi

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !

Mamlaka ya elimu ya ufundi Tanzania (VETA) kwa kushirikiana Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kupitia application ya VSOMO leo wametangaza na kuzindua kozi mpya za ufundi stadi za VETA zitakazotolewa  kupitia simu za mkononi ili kuwawezesha watanzania kujiunga na kupata utaalamu na vyeti vya VETA kwa gharama nafuu.


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Dk. Bwire Ndazi akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kozi tano mpya kwenye awamu ya pili ya mpango wa kutoa mafunzo ya ufundi stadi kupitia programu ya VSOMO inayoratibiwa na kampuni ya Airtel, Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya Airtel, Beatrice Singano.

Kozi hizo mpya zinazoongezwa katika mfumo wa vsomo ni  Huduma ya chakula na mbinu za kuhudumia wateja, Matengenezo ya kompyuta,umeme wa viwandani, ufundi Bomba wa Majumbani na Umeme wa magari.
Tangu kuzinduliawa kwa mfumo huu wa mafunzo kwa njia ya mtandao kupitia application ya VSOMO mwezi wa Juni 2016 ulianza kutoa kozi mbalimbali za ufundi za VETA ikiwemo Ufundi umeme wa manyumbani, Ufundi pikipiki, Ufundi wa simu za mkononi, Ufundi Alluminium,  Utaalamu wa maswala ya urembo pamoja ma Ufundi wa kuchomea vyuma. 
Lengo la mfumo huu likiwa ni kutimiza dhamira ya VETA ya kutanua wigo wa mafunzo ya ufundi stadi nchini na kuongeza idadi ya vijana kujipatia fani mbalimbali za ufundi ili waweze  kuajirika  au kujiajiri.  Mafunzo haya yanawawezesha wanafunzi kujisomea wakati wowote kwa gharama nafuu kupitia simu zao za mkononi za Airtel
Mfumo huu wa masomo kwa njia ya Mtandao VSOMO,  sasani maarufu kwa vijana ambapo takwimu zinaonyesha zaidi ya vijana 30,000 tayari wamepakua application ya VSOMO, 8000 wamejiandikisha na kati yao 50 wanasoma kozi mbalimbali zilizopo pia wapo waliomaliza na kupata vyeti vya VETA.

Akiongea wakati wa kuzindua na kutangaza kozi hizo, Mkuu wa Chuo cha Veta Kipawa, Mhandisi Lucius Luteganya alisema “mafunzo ya ufundi kwa njia ya mtandao ya VSOMO yametuwezesha kuongeza wigo na kuwafikia watanzania wengi nchini. Tunaamini bado tunayofursa ya kuongeza wigo  zaidi na kuongeza idadi ya vijana wenye ueledi ili kwenda sambamba na agenda ya serikali ya awamu tao ya uchumi wa viwanda kwa kupata nguvu kazi yenye taaluma muhimu katika kuendesha uchumu wa nchi”

“Tunaamini kozi hizi mpya zitatawavutia vijana wengi kujiandikisha, kusoma na kupata ujuzi zaidi.”  Alisisitiza Eng Luteganya

Luteganya alisema kuwa  “Ili kupata mafunzo ya VSOMO kupitia Airtel, ukiwa na Airtel pakua application katika google play store, na kujisajiri na kisha chagua kozi inayokidhi mahitaji yao. ili kuhakikisha tunasimamia viwango vya elimu vilivyowekwa na VETA, wale watakaomaliza masomo yao nadharia kupitia VSOMO watafanya mtihani ili kufaulu na kujiunga na mafunzo ya vitendo katika vituo vya VETA vilivyopo nchi nzima. Vyeti vya kuhitimu mafunzo vitatolewa kwa wale watakaofaulu mafunzo katika hatua zote mbili ya nadharia na vitendo”.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya alisema “Tunajisikia furaha kuongeza kozi nyingi zaidi katika mfumo huu  wa masomo kwa njia ya mtandao wa VSOMO  kwani itatuwezesha kufikia idadi kubwa ya vijana wanaosoma kwa kupitia simu zao za mkononi. Lengo letu ni kuhakikisha tunakuwa na kozi nyingi ili kwenda sambamba na matarajio na mahitaji ya wanafunzi na watanzania kwa ujumla"

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger