William Shao
Leo wamenivutia tena na uandishi, uchambuzi, uchaguzi, usanifu, utiririshaji na ubunifu wa gazeti Mtanzania Toleo Na. 8580 la leo, Juni 18, 2017. Mvuto wa kwanza, linasema: "Barrick wanapokuwa ndani ya mazungumzo, hupeleka watu wabobezi na hutumia mbinu inayojulikana kama ‘The Diplomatic-War Strategy’ ambao una msingi wa falsafa ya ‘Negotiate While Advancing’."
Chini ya kichwa cha habari "Serikali ikune kichwa," MTANZANIA limeandika: “…Acacia, imeonekana KUTAKA kupeleleza … timu ya kuiwakilisha Tanzania kwenye mazungumzo ya kutatua mgogoro wa mchanga…” Kwanini? Mtanzania linasema ni “…kujua nguvu na udhaifu wa—si tu mjumbe mmoja mmoja bali—timu nzima.”
Rais John Magufuli (katikati) akipokea ripoti ya madini kutoka kwa Profesa Nehemiah Osoro.
Kwa orodha na uchambuzi—jumlisha na majina ya wale watu waliotajwa na gazeti hilo ambao ni washauri na wawakilishi wa Barrick—ni dhahiri Mtanzania linadokeza kuwa sasa Tanzania iko vitani dhidi ya mabepari na mabeberu.
Hapa ndipo nilipovutiwa na ubunifu na usanifu wa ile headline “Serikali ikune kichwa timu ya kupambana na Barrick.”
Kama hivyo ndivo, hao mabepari na mabeberu hawaji kupambana na Chadema, CCM au CUF. Wanakuja wanapambana na Tanzania.
Kuna haja na ulazima wa kuachana na zile siasa zilizotufikisha hapa. Huwa tunapigana vita ya panzi ndiyo maana kunguru wanafurahi. Kusingekuwa na vita ya panzi tusingekuwa hapa tulipo.
Karibu nusu ya export yote ya Tanzania ni madini yetu. Na ingawa Tanzania ni nchi ya tatu kwa uzalishaji wa madini katika Afrika, wananchi wake hawanufaiki nayo—si kwa sababu ya hao wachimbaji—bali ni kwa sababu ya wale waliotutungia sheria zilizotoa mianya hii.
Nasi tuanze kuwachunguza walivyo kabla ya kukutana nao. Mmoja wa waliotajwa na gazeti hilo ni William Cohen ambaye amewahi kuwa Waziri wa Ulinzi wa Marekani (1997–2001) chini ya Bill Clinton.
Ni mwandishi mzuri sana vitabu na aliwahi kuwa Mwandishi wa Habari za Uchunguzi. Baadhi ya vitabu vyake ni Dragon Fire, Blink of an Eye © 2012, ‘Collision’ © 2011, ‘Roll Call: One Year in the United States Senate’ © 1981, ‘Double Man’ © 1986, ‘Biological Weapons: Limiting the Threat’ © 1999, ‘Preventing Genocide: A Blueprint for U.S. Policymakers © 2008, ‘Men of Zeal: A Candid Inside Story of the Iran-Contra Hearings’ © 1988, ‘Murder in the Senate’ na vingine kadhaa. Hao ndio hao. Si watu wa kusoma na kuchimbua mambo, bali wanaandika pia.
Inawezekana hawa wa aina ya huyu, au watu wengine watakaoshauriwa na hawa—ndio watapambana na timu yetu? Nakubaliana na ushauri wa gazeti MTANZANIA: "Serikali ikune kichwa,"
Sehemu moja ya mbinu ile iliyotajwa na gazeti hilo inasema hivi: “It would be helpful to know beforehand which kind of negotiator you face.
The difficulty is that skilful warriors will make themselves masters of disguise: at first they will seem sincere and friendly, then will reveal their warrior nature when it is too late.
In resolving a conflict with an enemy you do not know well, it is always best to protect yourself by playing the warrior yourself: negotiate while advancing.
There will always be time to back off and fix things if you go too far. But if you fall prey to a warrior, you will be unable to recoup anything.”
Kama mbinu itakayotumiwa na hawa jamaa ndiyo hiyo iliyotajwa na gazeti hili, then kitakachofanyika ni kwamba wataweka mashinikizo.
Watakuwa 'wagumu' na wasiolegeza mambo—na yote haya yatasindikizwa na kushindiliwa na hoja ngumu za kisheria na kibiashara.
Wao ni wazoefu katika hili kuliko tunavyoweza kukiri, na ndiyo maana Alhamisi ya Machi 22, 2018 Pakistani watasomewa hasara waliyoisababishia Barrick.
Shauri la Barrick dhidi ya Pakistan sasa liko Kituo cha Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji cha Benki ya Dunia (ICSID). Ni kiasi gani watakacholipa? Ni mabilioni ya dola.
Tusiwalaumu hao tunaowaita ‘wezi’, tujilaumu sisi wenyewe kwa kushangilia tusiyoyajua wakati baadhi ya viongozi wetu—nasema baadhi—wakituuza.
Mambo haya yaliwahi kuandikwa na wale tunaowapuuza. Wandishi wawili, Mark Curtis na Tundu Lissu, Machi 2008 walichapisha kijitabu walichokiita: "A Golden Opportunity: How Tanzania is Failing to Benefit from Gold Mining" © 2008.
Huyo aliyeandika hicho kitabu akishirikiana na Lissu ni mwandishi na mwanahistoria anayeheshimika sana na Waingereza. Kuna vitabu kadhaa ameandika. Tuvitafute maadamu vinapatikana.
'The Great Deception: Anglo-American Power and World Order' © 1988, 'Trade for Life: Making Trade Work for Poor People' © 2001, 'Web of Deceit: Britain's Real Role in the World' © 2003, 'Unpeople: Britain’s Secret Human Rights Abuses' © 2004.
Angalau basi Curtis au Tundu Lissu tujifanye—hata kama hatutaki—wawe kama yule aliyetajwa katika Mhubiri 9:15.
“Basi, kulionekana humo mtu maskini mwenye hekima, naye kwa hekima yake akauokoa mji ule lakini hata hivyo hapakuwa na mtu ye yote aliyemkumbuka yule mtu maskini.”
"Be sure you are right, then go ahead," alijisemea jemadari wa vita wa Marekani katika karne ya 18. Hongera tena gazeti ‘MTANZANIA’ kwa mara nyingine kwa uchambuzi wako.
Nawaombeni radhi kwa andiko reeeeeefu.
Wasalaam
SHARE









No comments:
Post a Comment