Mchora vibonzo Musa Ngarango aka “Masikio Mchongoko”, akilamba ganda lake.
Mchora vibonzo chipukizi, Brenda Kibakaya alidhihirisha kuwa uchoraji vibonzo si kwa wanaume tu.
Magret
Liwembe akimkabidhi zawadi mgeni rasmi (karikacha cha mke wa balozi
iliyonakshiwa kwa saini za washiriki) kwa niaba ya washiriki wenzake.
Mchora vibonzo Simon Regis akitoa neno la shukrani kabla ya kukabidhiwa vyeti.
Baadhi ya karikacha zilizochorwa wakati wa mafunzo hayo.
Mwezeshaji
na mwenyekiti wa NMF akiwa na washiriki wakati wa mafunzo hayo kabla ya
mgeni rasmi kuwasili. Mafunzo hayo ya siku tatu yaliyofanyika jijini
Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wachora vibonzo wa “kizazi cha tatu,”
yalijikiti katika misingi ya uchoraji karikacha na katuni za maoni.
Balozi
na Mwakilishi wa Uswisi Afrika Mashariki, Arthur Mattli, akimkabidhi
cheti cha ushiriki wa “Warsha ya Uchoraji Karikacha & Vibonzo,”
Saidi Michael maarufu kama “Wakudata” hivi karibuni baada ya kushiriki
mafunzo ya kuwajengea uwezo yaliyoendeshwa na asasi ya Nathan Mpangala
Foundation (NMF) na kufadhiliwa na Ubalozi wa Uswisi nchini. Katikati ni
Mwenyekiti wa NMF, Nathan Mpangala.
SHARE
No comments:
Post a Comment