Mkuu wa Kampuni ya mawasiliano ya Zantel-Zanzibar, Bw. Mohamed Khatib Baucha (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe. Mwanajuma Majid Abdallah mifuko ya Saruji kwa kwa ajili ya waathirika wa mafuriko yaliyotokea hivi karibuni katika mkoa huo. Zoezi la makabidhiano ya msaada huo lilifanyika jana mkoani humo ambapo Zantel walitoa jumla ya mabati 350 na Saruji mifuko 350, vyote vikigharimu Sh. 13 milioni.
Mkuu wa Kampuni ya mawasiliano ya Zantel-Zanzibar, Bw. Mohamed Khamis Baucha (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe. Mwanajuma Majid Abdallah mabati kwa kwa ajili ya waathirika wa mafuriko yaliyotokea hivi karibuni katika mkoa huo. Zoezi la makabidhiano ya msaada huo lilifanyika jana kisiwani Pemba-Zanzibar ambapo Zantel walitoa jumla ya mabati 350 na Saruji mifuko 350, vyote vikigharimu Sh. 13 milioni.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe. Mwanajuma Majid Abdallah akiwakabidhi wakuu wa wilaya za mkoa huo mabati yalitolewa na Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel kwa ajili ya waathirika wa mafuriko yaliyotokea hivi karibuni katika mkoa huo. Zoezi hilo lilifanyika jana kisiwani Pemba-Zanzibar ambapo jumla ya mabati 350 na Saruji mifuko 350 kwa pamoja vilikabidhiwa na Kampuni ya Zantel. (Katikati) ni Mkuu wa Wilaya ya Chakechake Mhe. Salama Mbarouk Khatib na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Mkoani Mhe. Hemed Suleiman Abdallah.
SHARE
No comments:
Post a Comment