Shule tano kufaidika na vitabu vya sayansi vyenye thamani ya shilingi milioni 5
Mbeya;
Katika kuinua sekta ya elimu nchini , kampuni ya simu za mkononi ya
Airtel leo imetoa msaada wa vitabu vya sayansi vyenye thamani ya
shilingi milioni 15 kwa shule 5 za sekondari mkoani Mbeya.
Vitabu
hivyo vimetolewa na Airtel kwa kushirikiana na Tulia Ackson foundation
kwaajili ya shule za sekondari za Ikuti, Kayuki , Bujeli, Ntaba na Ikupa
Akiongea
wakati wa hafla ya kukabidhi vitabu, Naibu Spika Mh Dkt, Tulia Ackson
alisema aliwapongeza Airtel kwa kushirikiana na taasisi yake ya Tulia
Ackson ili kusaidia shule za sekondari zenye uhaba wa nyenzo za
kujifunzia mkoani Mbeya. Dr. Ackson alisema” ni muhimu kwa makapuni
binafsi ya umma kushirikiana katika kuinua sekta ya elimu nchini ili
kuweka mazingira bora kwa wanafunzi kujifunza na hivyo kuongeza uelewa
na kuwa na taifa lenye ueledi
Tumeshuhudia
uhaba mkubwa wa vitabu katika mashule ambapo uwiano upo kati ya kitabu
kimoja kwa wanafunzi 5 hadi 10. Tunaamini msaada huu tunaoutoa leo
utasaidia kuzalisha nguvukazi yenye ueledi itakayowawezesha kujiajiri au
kuajiriwa na kujenga uchumi wenye nguvu. Natoa wito kwa makapuni
mbalimbali kuungana nasi na kuzifikia shule zenye uhitaji wa vifaa vya
kufundishia nchini
Kwa
upande wake Meneja Mauzo mkoani Mbeya, Bartholomew Masatu alisema”
Airtel tunaamini jamaa iliyoelimika inajengwa kutoka katika shule zenye
vifaa vya kufundishia vyakutosha hususani vitabu. Ili kuwa na maendeleo
endelevu ni muhimu kuwekeza kwenye elimu na leo tunathibitisha dhamira
yetu kwa kutoa msaada wa vitabu katika shule hizi hapa Mbeya”.
Tunaamini msaada utachochea ufaulu mzuri katika masomo ya sayansi katika mkoa wetu.” Aliongeza Masatu
Kwa
upande wake Mwalimu Mkuu wa sekondari ya Kayuki Bi Bertha Sarufu Kwa
niaba ya shule zilizofaidika na msaada wa vitabu alisema “ Tunashukuru
sana Airtel kwa kutufikishia msaada huu na napenda kutoa wito kwa
wanafunzi kuvitunza na kuvitumia vitabu hivi kwa lengo la kuboresha
ufaulu. Msaada huu umekuja wakati muafaka wakati shule zetu zimekuwa na
upungufu wa vitabu na tunaahidi kuvitunza na kuvitumia ipasavyo".
WAZIRI
wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako pamja na Naibu Spika wa Bunge,
Dkt.Tulia Akson wakipokea vitabu vya masomo ya sayansi vilivyotolewa
msaada na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel.Anayewakabidhi vitabu
hivyo ni Meneja mauzo wa Airtel mkoa wa Mbeya bw, Bartholomew Masatu.
Airtel imekabidhi vitabu hivyo mwishoni mwa wiki hii ikiwa ni ahadi yake
ya kuendeleza masomo ya sayansi nchini.
WAZIRI
wa Elimu Profesa, Joyce Ndalichako (Kushoto)akiwa na Naibu Spika wa
Bunge la Jamuhuri ya muungano wa Tanzania , Dkt.Tulia Akson ,
wakimkabidhi vitabu vya sayansi kwa Mkuu wa sekondari ya Kayuki, Bertha
Sarufu, vitabu vilivyotolewa msaada na kampuni ya simu za mkononi ya
Airtel. Mbali ya Kayuki, shule nyingine za sekondari zilizonufaika na
msaada huo ni Ikuti, Bujela, Ntaba na Ikapu, zote zipo wilayani Rungwe.
Airtel imekabidhi vitabu vya sayansi mwishoni mwa wiki vyenye thamani ya
shilingi milioni 15.
SHARE
No comments:
Post a Comment