Richard Kayombo
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
11 JULAI 2017
Mamlaka ya Mapato Tanzania imefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi trilioni 14.4 kwa mwaka wa fedha 2016/17.
Makusanyo haya ni sawa na ukuaji
wa asilimia 7.67 ikilinganishwa na makusanyo ya mwaka 2015/16 ambayo
yalikuwa ni kiasi cha Shilingi Trilioni 13.3.
Sambamba na Makusanyo, Mkurugenzi
wa Huduma na Elimu kwa Mlipa kodi TRA Bw. Richard Kayombo alisema
Mamlaka imeendelea kukusanya kodi mbalimbali ikiwemo kodi ya majengo na
muitikio wake umekuwa ni wa kiwango cha kuridhisha.
Mamlaka inapenda kuwashukuru
walipakodi wote kwa muitikio huo na wengine wanaoendelea kujitokeza
katika ofisi mbalimbali za Mamlaka nchi nzima ili kuweza kulipa kodi
hiyo ambayo mwisho wa kulipa kodi hiyo ni tarehe 15 Julai, 2017.
Aidha, Mamlaka inapenda kutoa wito kwa wafanyabiashara wote kutoa risiti za EFD pindi wanapo uza bidhaa au huduma na Wananchi wote kuhakikisha wanadai risiti pindi wanapo nunua bidhaa au huduma na kwa, kinyume na hapo hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yeyoteatakayekutwa na kosa la kutokudai ama kutokutoa risiti.
Hivi sasa kuna zoezi la uhamasishaji na ukaguzi linaloendelea nchi nzima katika sehemu zote za biashara kukagua wafanyabiashara wasiotumia Mashine za Risiti za Kielektroniki za EFDs pamoja na wananchi wote wasiodai risiti baada ya kununua bidhaa au huduma.
“Napenda kuwakumbusha wananchi
wote kuhakiki risiti zao ili kuona usahihi wa tarehe na kiasi
walicholipa kabla ya kuondoka na risiti hiyo” alisistiza Kayombo
‘Pamoja Tunajenga Taifa Letu’
Richard Kayombo
MKURUGENZI WA HUDUMA NA ELIMU KWA MLIPAKODI
SHARE
No comments:
Post a Comment