Visiwa
vya Zanzibar na Mauritius vina fursa ya kubadilishana uzoefu katika
miradi ya Maendeleo ili kujiongezea ujuzi na maarifa yanatayowawezesha
Wananchi wake kuimarika zaidi kiuchumi hali itakayosababisha Mataifa yao
kuongeza mapato.
Mwenyekiti
wa Kampuni ya Kimataifa ya Ushauri kutoka Kisiwa cha Mauritius { Moneo
Consulting } Bwana Devanand Virahsawmy akiuongoza ujumbe wa viongozi wa
Kampuni hiyo alisema hayo wakati wa mazungumzo yake na Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Balozi Seif Vuga Mjini Zanzibar.
Bwana
Devanand Virahsawmy alisema Sekta ya elimu ambayo ndiyo mama katika
Taifa lolote Duniani inaweza kuwa mwanzo wa ushirikiano huo unaoweza
kutoa nafasi kwa vijana wa pande hizo mbili kujipatia Elimu ya Msingi,
Sekondari hadi vyuo Vikuu .
Alisema
mpango huo wa pamoja kupitia Kaisheni ya pamoja kwa Nchi
zilizozunguukwa na Bahari ya Hindi utaongeza chachu ya uchumi kwa Vijana
waliobobea Kitaaluma sambamba na ongezeko la ajira.
Bwana
Devanand alisema Visiwa vya Mauritius tayari vimeshapiga hatua kubwa ya
maendeleo hasa katika Sekta ya Utalii kiwango ambacho wanaweza kusaidia
Taaluma kwa Nchi zilizo jirani na Visiwa hivyo.
Mwenyekiti
huyo wa Kampuni ya Moneo Consulting alimueleza Balozi Seif pamoja na
Mawaziri, Makatibu Wakuu na Watendaji Wakuu wa SMZ Kwamba Uongozi wa
Kampuni yake upo Zanzibar kuitika wito Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
wa kuangalia fursa za Uwekezaji.
Alieleza kwamba Kampuni hiyo tayari imeshijengea uwezo wa kuendesha
miradi mbali mbali ya Kiuchumi na Maendeleo akiitaja baadhi yake kuwa ni
pamoja na Miradi ya Umeme, Bara bara, Utalii, Benki ya Ufukweni { Off
show Bank } Viwanda vya vidogo vidogo pamoja na Uvuvi wa Bahari Kuu.
Akitoa ufafanuzi wa mipango ya Uwekezaji Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Uwekezaji Vitega Uchumi Zanzibar {ZIPA} Nd. Salum Nassor Khamis alisema
Zanzibar imeanza kufanya mabadiliko ya uchumi wake katika Miaka ya 90
ili kutoka nafasi kwa Taasisi yenye uwezo wa uwekezaji kushiriki kwenye
mabadiliko hayo.
Ndugu Salum alisema ushirikishwaji wa Sekta binafsi katika kuchangia
uchumi wa Taifa umezingatiwa ili kujenga jamii itakayokwenda sambamba na
mabadiliko ya Kiuchumi Duniani.
Naye kwa upande wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali
Iddi aliueleza Ujumbe huo wa Kampuni ya Ushauri ya Moneo kwamba Zanzibar
ina mtazamo wa kuwekeza katika sekta ya Uvuvi wa Bahari Kuu.
Alisema Rasilmali ya Bahari ni eneo linaloweza kujenga uchumi imara
utakaoweza kuongeza mapato ya Taifa sambamba na kupunguza ufinyu wa
ajira uliowakumba Vijana wengi wanaomaliza masomo yao Nchini.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
24/7/2017.


SHARE
No comments:
Post a Comment