Mwimbaji
maarufu wa muziki Bongo, Baraka Da Prince aliyesaini mkataba wa kufanya
kazi na label ya Rockstar 4000 mwaka jana 2016, ameamua kuachana na lebo
hiyo huku akibainisha sababu za kufanya maamuzi hayo magumu.Akizungumza Julai 21, 2017 kupitia kipindi cha XXL, Baraka amethibitisha kuwa
hayupo tena chini ya Rockstar4000 na kuwa anafanya kazi zake binafsi
akidai kuna mambo hayapo sawa kati yake na menejimenti huku akisisitiza
siyo kwa sababu Alikiba amekuwa mmoja wa wakurugenzi wa label hiyo.
”Kuna
vitu lazima uvihoji na ukiona watu unaofanya nao kazi kama kampuni
wanakuwa hawajali kitu unachotaka kufahamu kuhusu makubaliano yenu ya
kazi inakuwa na mashaka kidogo”
“Naweza
kusema sipo chini ya Rockstar kwa sababu mimi ndio boss wa muziki wangu,
mimi ndio nafanya kazi, kukiwa na vitu havipo sawa kwa upande wangu
mimi ndio naweza kutoa kauli ya mwisho, sipo chini ya Rockstaar”
“Kuna
vitu haviko sawa hilo neno boss zito sana, unaponiambia mtu ni boss
wangu, how? Boss kivipi kwangu? Alikiba kuwa director wa Rockstar mimi
ndio nijitoe, hapana…. kuna vitu havipo sawa na uongozi wa Rockstar”
“Nilipokwenda
Rockstar4000 sikusaini chini ya AliKiba, mimi nina matatizo binafsi na
uongozi na kama mambo hayapo sawa ukiona kitu jua kipo chini ya Baraka,”
alisema Baraka the Prince.
SHARE
No comments:
Post a Comment