Spika
wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Job Ndugai ambaye pia ni
mbunge wa Jimbo la Kongwa, akisalimiana na Mkurugenzi wa Tawi la Benki
ya CRDB Dodoma, Bi. Rehema Hamisi wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa
mifuko 200 ya Saruji iliyotolewa na Benki ya CRDB kwa ajili ya kusaidia
Ujenzi wa Nyumba ya Walimu wa shule hiyo iliyopo jimboni kwake Kongwa
mkoani wa Dodoma.
Spika
wa Bunge, Job Ndugai, akisalimiana na Meneja wa Kituo cha Huduma kwa
Wateja Njia ya Simu (Call Center), Ena Mwangama, wakati alipowasili
katika Shule yua Sekondari ya Laikala.
Spika wa Bunge, Job Ndugai na Mkurugenzi wa Tawi la Benki ya CRDB Dodoma, Rehema Hamisi wakielekea shuleni hapo.
Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Tawi la Dodoma,
Rehema Hamisi (wa pili kushoto), akipiga ngoma sambamba na wasanii wa
kikundi cha Matumaini kilichokuwa kikitumbuiza katika hafla hiyo.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Laikala, Msafiri Simon, akisoma historia fupi ya shule hiyo.
Mkurugenzi waBenki ya CRDB Tawi la Dodoma,
Bi. Rehema Hamisi, akisoma hotuba katika hafla ya kukabidhi msaada wa
mifuko 200 ya Saruji iliyotolewa na Benki ya CRDB kwa ajili ya Kusaidia
Ujenzi wa Nyumba ya Walimu katika Shule ya Sekondari Laikala.
Baadhi
ya walimu na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Laikala wakisikiliza
hotuba ya Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Tawi la Dodoma, Rehema Hamisi.
Spika wa Bunge, Job Ndugai, akizungumza katika hafla ya Benki ya CRDB kukabidhi mifuko 200 ya saruji.
Baadhi
ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Laikala wakimsikiliza Spika wa Bunge
na mbunge wa Jimbo la Kongwa, Job Ndugai wakati shule hiyo ilipopokea
msaada wa Sh. Milioni 15 kutoka Benki ya CRDB kwa ajili ya kuboresha
miundombinu ya shule hiyo.
Spika
wa Bunge, Job Ndugai, ambaye pia ni mbunge wa Kongwa, akipokea mfano wa
hundi ya Sh. Milion 15 kutoka kwa Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Tawi laDodoma,
Rehema Hamisi kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa nyumba ya walimu katika
Shule ya Sekondari Laikala iliyopo wilayani Kongwa. Kulia ni Diwani wa
Kata ya Sagala, Simon Kamando, akishuhudia.
Spika
wa Bunge, Job Ndugai (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na
wafanyakazi wa Benki ya CRDB Tawi la Dodoma pamoja na viongozi
mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo.
Wanafunzi wakifurahia mfano wa hundi iliyotolewa na Benki ya CRDB.
Sehemu ya mifuko ya sarui iliyokabidhiwa na Benki ya CRDB kwa Shule ya Sekondari Laikala.
Spika
wa Bunge, Job Ndugai, akitoa shukrani zake kwa Benki ya CRDB baada ya
kupokea mifuko 200 ya saruji pamoja na hundi ya Sh. Milioni 15.
Baadhi
ya wageni waalikwa wakiwa katika hafla ya makabidhiano ya hundi ya Sh.
Milioni 15 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa nyunba ya walimu pamoja na
kuboresha miundombinu katika Shule ya Sekondari Laikala.
Baadhi ya maofisa wa Benki ya CRDB.
Baadhi ya wananchi wakifuatilia hafla ya makabidhiano ya mifuko ya saruji.
Baadhi ya maofisa wa Benki ya CRDB wakiwa katika hafla hiyo.
SHARE
No comments:
Post a Comment