Waziri
Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi waiyo hudhuria katika
maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtukufu Agakhan alipo chaguliwa kuwa Imamu
mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani, akiwa amemuwakilisha Rais
Dkt. John Magufuli, Julai 9, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi waiyo hudhuria katika
maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtukufu Agakhan alipo chaguliwa kuwa Imamu
mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani, akiwa amemuwakilisha Rais
Dkt. John Magufuli, Julai 9, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu,Kassim Majaliwa akisalimiana na mama Zakia Megji wakati wa
maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtukufu Agakhan alipo chaguliwa kuwa Imamu
mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani, akiwa amemuwakilisha Rais
Dkt. John Magufuli, (kushoto) ni Rais wa Jumuiya ya Shia Ismailia Amin
Lakhani Julai 9, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu,Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Jumuiya ya Shia Ismailia
Amin Lakhani wakati wa maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtukufu Agakhan
alipo chaguliwa kuwa Imamu mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani,
akiwa amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli, (katikati) ni Mkuu wa
Wilaya ya Ilala Sofia Mjema Julai 9, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Waziri
Mkuu,Kassim Majaliwa akipokea shada la maua wakati akikaribishwa kwenye
maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtukufu Agakhan alipo chaguliwa kuwa
Imamu mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani, akiwa amemuwakilisha
Rais Dkt. John Magufuli, (katikati) ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sofia
Mjema Julai 9, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu,Kassim Majaliwa akisaini kitabu cha wageni kwenye maadhimisho ya
miaka 60 tangu Mtukufu Agakhan alipo chaguliwa kuwa Imamu mkuu wa
madhehebu ya Shia Ismailia duniani, (kushoto) ni Rais wa Jumuiya ya Shia
Ismailia Amin Lakhani na (kulia) ni muwakilishi wa AKDN Resident Amin
Kurji, wakati alipomwakilisha Rais Dkt. John Magufuli, (katikati) ni
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sofia Mjema Julai 9, 2017. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza na Muwakilishi wa AKD resident Amin
Kurji katika maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtukufu Agakhan alipo
chaguliwa kuwa Imamu mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani,
yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, akiwa amemuwakilisha
Rais Dkt. John Magufuli,(katikati) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali
ya Aga Khan Suleiman Shabbudin Julai 9, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Waziri
Mkuu,Kassim Majaliwa akiteta jambo na Rais wa Jumuiya ya Shia Ismailia
Amin Lakhani, katika maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtukufu Agakhan alipo
chaguliwa kuwa Imamu mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani, akiwa
amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli, Julai 9, 2017.
Waziri
Mkuu,Kassim Majaliwa akipokea maandano ya maadhimisho ya miaka 60 tangu
Mtukufu Agakhan alipo chaguliwa kuwa Imamu mkuu wa madhehebu ya Shia
Ismailia duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Diamond Jubilee,
Waziri Mkuu amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli katika sherehe hiyo,
Julai 9, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
……………………………………………………………..
*Asema nchi ina utulivu wa kisiasa na uchumi unaokuwa kwa kasi
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amewahakikishia uwekezaji wenye tija wawekezaji
watakaokuja nchini kwa kuwa Tanzania ni nchi yenye amani, utulivu wa
kisiasa na uchumi wenye kukua kwa kasi.
Ameyasema
hayo leo (Jumapili, Julai 09, 2017) alipomuwakilisha Rais Dkt. John
Magufuli katika maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtukufu Aga Khan
alipochaguliwa kuwa Imamu Mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani.
Waziri
Mkuu amesema Serikali inatambua na kuthamini shughuli mbalimbali
zinazofanywa na mtandao wa taasisi za Aga Khan zilizopo hapa nchini,
hivyo Serikali itaendelea kushirikiana nao.
Ameupongeza
mtandao wa taasisi za Aga Khan kwa kumuunga mkono Rais Dkt. Magufuli
katika kutoa kipaumbele cha kuwapa fursa watu wenye kipato cha chini
kushiriki katika uzalishaji ili waweze kujikwamua kiuchumi.
“Nawahakikishia
kwamba uwekezaji wenu hapa nchini utakuwa na baraka kwa sababu nchi
imetulia kisiasa na uchumi wake unakua kwa kasi. Nawaomba muendelee
kuwaalika wanajumuia wa madhehebu ya Shia Ismailia popote walipo duniani
waje kuwekeza nchini fursa bado zipo.”
Kwa
upande wake Rais wa Jumuiya ya Madhehebu ya Shia Ismailia Tanzania, Bw.
Amin Lakhani ameishukuru Serikali kwa ushirikiano inaowapa na kwamba
ameahidi kuendelea kushirikiana nayo katika kuboresha sekta mbalimbali
nchini.
Amesema
mtandao wa maendeleo wa Aga Khan unatoa huduma mbalimbali zikiwemo za
afya, elimu, kilimo na kunaendesha miradi katika mabara ya Afrika na
Asia kwa kuwapa fursa watu wenye kipato cha chini kushiriki katika
uzalishaji ili kujikwamua kiuchumi.
Awali,
Mkuu wa wilaya ya Ilala, Bi. Sophia Mjema aliipongeza taasisi hiyo kwa
mpango wake wa upanuzi wa hospitali na kuongeza vituo 35 vya afya kutoka
15 walivyonavyo.
SHARE
No comments:
Post a Comment