Msanii wa hip hop Bongo, Chid Benz amemtaka msanii mwenzake Chin Bees kutafuta jina lingine.
Sababu
ya Chid Benz kusema hivyo imetokana na majina yao kufanana, na kuongeza
kuwa wote wanafanya muziki wa aina tofauti hivyo kulikuwa hakuna
ulazima wa ufanya hivyo.
“Siku
moja nimeona Shetta anamuangalia instagram nikamuuliza huyo ni nini?,
akaniambia ni Chin Bees, nikamuuliza anafanya muziki gani, akaniambia
Bongo Fleva!. Sisemi kwa ubaya ila sikuelewa ile style anayofanya yeye
ni tofauti sana na mimi mtu mzima mwenye hit kama 32 najua nikiingia
kwenye stage nachapa tu,” Chid Benz ameiambia Planet Bongo ya EA Radio
na kuhoji.
“Huyo Chin Bees ana single hata saba kweli?, atafute jina lingine,” amemaliza kwa kusema.
SHARE
No comments:
Post a Comment