Msanii
wa muziki wa asili ambaye pia ni Balozi wa Hifadhi ya Eneo la
Ngorongoro (NCAA), Mrisho Mpoto ametangaza deal kwa waimbaji pamoja na
wapiga ala za muziki kujitokeza kwa wingi Sabasaba jijini Dar es salaam
katika banda la maonyesho la Hifadhi ya Ngorongoro kwaajili ya kupata
wasanii wapya watakao unda bendi mpya ya hifadhi hiyo.
Akiongea
wa wadau waliojitokeza kwa wingi katika banda hilo, Mrisho Mpoto ambaye
ni balozi wa hifadhi hiyo, alisema vijana hao wanatakiwa kujua kuimba
pamoja na mambo mbalimbali yanayohusu Hifadhi ya Ngorongoro pamoja na
vitu vinavyopatikana.
“Hii
fursa kwa waimbaji wa muziki pamoja na wapiga ala za muziki, tunatakiwa
kuanzisha bendi ya muziki ‘Ngorongoro Band’, kuandaa nyimbo maalum
ambazo zitakuwa zinawaelimisha watanzania juu ya ufahari wa hifadhi hii.
Kuandaa wimbo ambazo zitawafanya watanzania kuijua zaidi mbuga zao ,
masuala ya utalii pamoja na vitu mbalimbali vilivyomo ndani yake,”
alisema Mpoto.
Katika
hatua nyingine Mrisho amesema anashukuru wadau mbalimbali wanajitokeza
kwa wingi katika banda la Ngorongoro kwaajili ya kujifunza mambo
mbalimbali kuhusu hifadhi ya Ngorongoro pamoja na wanyama wanaopatika.
“Kuwema
kweli mambo yamekuwa mazuri sana katika banda letu, watu wanakuja kwa
wingi sana kwa sababu sisi tunatoa burudani na elimu, burudani na elimu,
kuna bendi hapa In African ambio inatoa burudani kila siku, kuna mastaa
mbalimbali wanakuja kutoa burudani kama mlivyowana akina Stara Thomas,
Solid Ground, Steve B&B na wengine wengi ambao wanakuja na kuondoka.
Kwa hiyo kikubwa zaidi kwetu ni burudani na elimu,” alisema Mpoto.
Aliongeza,
“Pia tumekuwa na kipengele cha elimu kuhusu wanyama kila siku na baada
ya haps tunawaita watoto waeleze vitu ambavyo wanajifunza kila siku na
tumekuwa tukitoa zawadi ya mpaka tsh milioni moja kwa siku na tumeona
matunda kabisa watoto wanakuja hapa hawajuhi chochote lakini wakiondoka
hapa wanaweza kueleza vitu mbalimbali ambavyo vinapatika katika hifadhi
ya Ngorongoro,”
Mshairi
huyo amewataka watanzania kwa ujumla kutembelea banda hili pamoja na
watoto wao ili wapate kujifunza mambo mbalimbali kuhusu Hifadhi ya
Ngorongoro.
SHARE
No comments:
Post a Comment