TRA

TRA

Tuesday, July 4, 2017

Daah! wizi hatari kweli. Wachomwa moto kisa wizi wa pikipiki

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !



Wananchi waliojichukulia sheria mkononi wamewaua kwa kuwachoma moto watu watatu ambao majina yao bado hayajafahamika katika kijiji cha Kitwana kata ya Busoka wilayani Kahama,mkoani Shinyanga kwa tuhuma za wizi wa pikipiki.

Kwa mujibu wa mashuhuda, mauaji ya mtu wa kwanza yamefanywa majira ya saa nane usiku wa kuamkia leo baada ya kutokea wizi wa pikipiki, huku watu wengine wawili wakiuawa leo majira ya saa nne asubuhi.

Inaelezwa kuwa mtuhumiwa wa kwanza alipokamatwa aliwataja wenzake wawili waliouawa jana baada ya kuvunja nyumba ya mmoja wao na kukuta pikipiki tatu zimehifadhiwa kwenye shimo.

Afisa mtendaji wa mtaa wa Kitwana, Peter Joseph amekiri kutokea kwa tukio hilo huku akilaani vikali kitendo cha wananchi kujichulia sheria mkononi, na kuwataka kuacha tabia hiyo kwani ni kinyume cha sheria.

Miili ya marehemu hao imechukuliwa na Jeshi la polisi wilaya ya Kahama, na kupelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Kitwana,Peter Joseph akiwa katika eneo ambalo watu hao wamechomwa moto

Nyumba ya mmoja wa watuhumiwa ikiendelea kuwaka moto,katikati ni pikipiki iliyokutwa kwenye shimo la choo ikichomwa.

Baadhi ya waendesha boda boda na wananchi wakiwa katika eneo la makazi ya mmoja wa watuhumiwa wakishuhudia nyumba ikiteketea.

Mkuu wa polisi wilaya ya kahama Mussa Mchenya mwenye kofia nyeusi akiwa eneo la tukio akishuhudia eneo ambalo watuhumiwa hao wamechomewa moto.

Wananchi wakiwa katika makazi ya mtuhumiwa aliyechomwa moto wakishuhudia nyumba ikiteketea.

Nyumba ikiendelea kuteketea eneo la Sofia Kahama.

Baadhi ya waendesha bodaboda na wananchi wakiangalia nondo iliyochongwa ambayo inahisiwa kutumika katika mauaji ya madereva boda boda.

Afisa wa jeshi la polisi akiendesha pikipiki ya mmoja wa mwendesha boda boda ambayo alikutwa eneo la tukio na kukamatwa kwa lengo la kusaidia polisi.

Maafisa wa polisi wakiwa eneo la tukio

Shimo ambalo mtuhumiwa inadaiwa alificha pikipiki tatu ndani yake.

Wananchi wakiendelea kubomoa nyumba ya mtuhumiwa

Askari polisi wakiwa katika eneo la tukio baada ya kuchukua miili ya watuhumiwa waliochomwa moto.

Maafisa wa polisi wakiwa wameifikisha miili ya watuhumiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya wilaya ya Kahama.
Picha zote na mwandishi wa Malunde1 blog - Kahama

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger