Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM umekuwa mji mwenyeji katika mfululizo wa mkutano mkuu wa kampuni za simu za mkononi wa GSMA 360 kwa mara ya pili mfululizo.
Mkutano huo ambao huleta pamoja wadau wa sekta ya mawasiliano ya simu, huzunguka katika miji tofauti katika masoko muhimu duniani kote na umerejea tena Dar es Salaam mwaka 2017 baada ya kufanyika nchini kwa mara ya kwanza mwaka jana.
Ian Ferrao
Mfululizo wa mikutano ya kampuni za simu za mkononi wa GSMA 360 ni jukwaa la mikutano linalokuza ushirikiano wa kikanda kwa kuzungumzia mada zinazoathiri sekta ya simu ndani na nje ya nchi.
Watendaji waandamizi wa vituo mbalimbali vya simu za mkononi na wa sekta jirani wanakuja kujifunza na kujadili kwa undani changamoto na mafanikio yao kwa ujumla huku wakiboresha uhusiano baina ya washiriki.
Akizungumzia kwa kuwa mdhamini mkuu na mikakati waliyonayo juu ya mkutano huo wakati wa sherehe ya ufunguzi kwa mwaka 2017, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao alisema:
"Mfululizo wa mikutano ya simu za mkononi wa GSMA 360 Afrika hukutanisha viongozi katika nchi za Jangwa la Sahara ili kutathimini ufikiwaji na uingizwaji wa mfumo wa kidijitali, ufikiwaji wa mtandao na ubora wa hali ya juu kwa wateja".
Aliongeza kuwa, "tuna siku tatu za kujifunza kutoka kwa kila mmoja wetu na kuendelea kuthibitisha juhudi zetu za ushirikiano katika kubadilisha maisha ya Waafrika, ili kuwa na jamii bora,".
"Ikiwa ndiyo kampuni inayoongoza kwa kutoa ufumbuzi wa mawasiliano wakati wote, mfano sauti (voice), data, uunganishwaji, au suluhisho la satelaiti, ni fursa kubwa kwa Vodacom Tanzania kuwa mfadhili mkuu wa mkutano huu," alisema Ferrao.
SHARE
No comments:
Post a Comment