Mkuu
wa Wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro amewataka wakazi wa mjini
Shinyanga kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu ili waweze
kupata elimu wakiwa katika mazingira rafiki na kupata ufaulu mzuri ambao
utawafanya wafikie malengo yao ya maisha.
Matiro
amesema anasikitishwa na wananchi mjini Shinyanga kuwa wa kwanza
kuchanga michango ya harusi na wengine kutumia pesa hovyo kwenye vileo
na wakati kuna watoto wanahitaji msaada hata wa sare za shule na viatu
ili waende shule lakini kutokana na kuishi mazingira magumu watoto
wanakwama na hatimaye kufanya vibaya darasani.
Matiro
ametoa rai hiyo leo Alhamis Julai 6,2017 mjini Shinyanga wakati
akikabidhi nguzo za shule kwa watoto 164 kati ya 1400 ambao wanaishi
katika mazingira magumu katika manispaa ya Shinyanga.
Matiro
ametoa msaada huo kwa kwshirikiana na Shirika la TVMC na PWWCO ambayo
yanasaidia watoto na akina mama wanaoishi katika mazingira magumu mjini
Shinyanga.
Matiro
alisema lengo kuu la msaada huo kuuonesha umma kuguswa namna ya
kusaidia watoto wanaoishi mazingira hayo na siyo kuiachia serikali peke
yake zikiwamo NGO's na Wageni kutoka nje ya nchi kuja kuokoa watoto hao
na wakati wananchi nao wana uwezo wa kuwatatulia changamoto hizo.
"Ukipita
mchango wa harusi unakuta watu wanakuwa wa kwanza kuchangia tena kwa
haraka lakini likija suala la kusaidia watoto wanaoishi mazingira
magumu, kila mtu utasikia akisema hana pesa ,wananchi mnatakiwa
mbadilike" alisema Matiro.
Naye
mkurugenzi wa Shirika hilo la TVMC Mussa Jonas Ngangala alisema
walifanya utafiti wa kubaini watoto wanaoishi katika mazingira magumu
Aprili mwaka huu kwa kushirikiana na wenyeviti wa mitaa na watendaji
katika kata zote 17 za manispaa ya Shinyanga ambapo walipata watoto hao
1400 na katika awamu ya kwanza wamesaidia watoto 164 huku wakitarajia
pia kufungua kituo cha watoto wanaoishi katika mazingira magumu mjini
Shinyanga.
Alisema
changamoto ambazo zimekuwa zikiwakabili kwenye zoezi hilo la kutambua
watoto wanaoishi katika mazingira magumu kuwa ni baadhi ya wenyeviti wa
mitaa kugomea kufanya zoezi hilo kwa madai ya kutaka posho kwanza na
hivyo kujikuta hapo mwanzo wakipatiwa watoto ambao sio wahusika ambapo
waliwakataa na kufanya mchakato upya na kuwapata watoto sahihi.
Ngangala
alisema zoezi la kutambua watoto wanaoishi katika mazingira magumu
katika kata ya Shinyanga Mjini liliaharishwa kwa sababu ya viongozi wa
serikali za mitaa kutaka posho na kugomea zoezi hilo.
Kwa
upande wake Ofisa elimu shule ya msingi manispaa ya Shinyanga Yesse
Kanyuma alisema msaada wa nguo hizo utasaidia wanafunzi hao kufanya
vizuri katika masomo yao ikiwa mtoto anaposoma katika mazingira magumu
kamwe hawezi kufanya vizuri sababu akili yake haitakuwepo darasani na
kuanza kuwaza wapi atapata chakula sambamba na mavazi yake kuchakaa na
hivyo kumuhamisha kabisa darasani na kutomuelewa mwalimu.
Mkurugenzi
wa Shirika la TVMC mjini Shinyanga Mussa Jonas Ngangala akisoma taarifa
kwa mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro jinsi shirika hilo
linavyosaidia watoto wanaoishi katika mazingira Magumu na malengo yao
juu ya kusaidia watoto 1,400 wanaoishi katika mazingira magumu katika
manispaa ya Shinyanga
Mkurugenzi
wa Shirika la TVMC mjini Shinyanga Mussa Jonas Ngangala akisoma taarifa
kwa mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
Mkuu
wa Wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akigawa sare za shule kwa
watoto 164 wanaoishi katika mazingira magumu katika manispaa ya
Shinyanga
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akimkabidhi sare ya shule mwanafunzi
Zoezi la kukabidhi sare za shule likiendelea
Mwanafunzi akipokea sare za shule
Zoezi la kukabidhi sare za shule likiendelea
Watoto
164 wanaoishi katika mazingira magumu wakiwa wamekaa wakisubiri kupewa
msaada wa sare za shule na mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Josephine
Matiro.
Mkuu
wa Wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwa na mtoto anayeishi kata
ya Ibadakuli na kusoma shule ya msingi Viwandani mjini Shinyanga ambaye
anaishi katika mazingira magumu na bibi yake ambaye naye ni mgonjwa na
amekuwa akigeuka kuwa mlezi wa familia ambapo akitoka shule anachukua
panga na kwenda kuchanja kuni na kuuza ili apate pesa ya kula yeye na
bibi yake, jambo ambalo lilimgusa mkuu huyo wa wilaya na kuamua
kumchangishia pesa pamoja na kumtafutia wadau wa kusaidia familia yake
ikiwemo chakula, afya ,mavazi na elimu sambamba na kukarabati nyumba
ambayo anaishi na bibi yake
Mtoto huyo akielezea historia ya maisha ambapo wadau waliguswa na kutoa misaada mbalimbali
Mkuu
wa Wilaya Shinyanga Josephine Matiro akimkabidhi nguo za shule mtoto
huyo ambaye anaishi na bibi yake,na yeye ndiye mlezi wake. Ofisa
Utumishi wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Magedi Magezi alitoa
shilingi 30,000 kwa ajili ya kumnunulia viatu mtoto huyo.
Michango
ya fedha ikiendelea ili kumsaidia mtoto ambapo jumla ya fedha Shilingi
195,600 zilipatikana pamoja na ahadi ya vyakula kila wiki na wengine
kila mwezi kuahidi kusaidia familia hiyo
Mchungaji
wa Kanisa la Wasabato mjini Shinyanga John Kilinda akitoa shilingi
300,000 huku Mwezake wa kanisa la Wasabato Lubaga Elias Nyangusu
akiahidi kukarabati nyumba anayoishi mtoto huyo.
Mwenyekiti
wa makanisa ya kipentekoste mkoa wa Shinyanga Askofu Elias Madoshi
kutoka kanisa la FPCT akiahidi kuchukua watoto 10 ambao wanaishi katika
mazingira hayo magumu na kuwasaidia kielimu na huduma zote huku akiahidi
kutoa gunia la mchele kwenye familia ya mtoto anayeishi na bibi yake
Naye
mfanyabishara wa maduka ya nguo za kisasa mjini Shinyanga Ommy Fashion
(aliyevaa miwani kulia) hakuwa nyuma kutoa mchango kusaidia watoto
wanaoishi katika mazingira hayo magumu ambapo alitoa shilingi 200,000.
Mkuu
wa Wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akimkabidhi Ofisa Elimu kata ya
Ibadakuli Alphonsina Sendaye fedha zilizochangwa na wadau na kutoa
maagizo zitumike kwa madhumuni yaliyokusudiwa kumsaidia mtoto huyo
Wazazi na walezi wa watoto hao wakiwa eneo la tukio
Wazazi
,walezi na viongozi mbalimbali wa serikali wakishuhudia tukio hilo la
ugawaji sare za shule kwa watoto hao wanaoishi katika mazingira magumu.
Picha zote na Marco Maduhu- Malunde1 blog
SHARE
No comments:
Post a Comment