Waziri wa Fedha na Mipango, Philip Isdor Mpango (Mb) akiongea na mmoja wa wananchi
(anayemuonesha karatasi ) waliofika kulipa kodi ya majengo katika ofisi
za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) – Kigamboni, ambapo alieleza
kuridhishwa na utendaji wa watumishi katika mamlaka hiyo.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Isdor Mpango (Mb), aliyevaa miwani na kukunja mikono, akiwa
amejichanganya katika kundi la wakazi wa mji wa Kigamboni waliojitokeza
kulipa kodi ya majengo katika Ofisi za Mamlaka ya Mapato
Tanzania-Kigamboni, akiwa na lngo la kuchunguza namna wananchi
wanavyopata huduma.
Waziri wa Fedha na Mipango,Dk. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akisalimiana na mmoja wa wakazi
wa Mji wa Kigamboni waliojitokeza kulipa kodi katika Ofisi za mamlaka ya
mapato Tanzania TRA-Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk.
Philip Mpango (Mb), akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Msaidizi wa
Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Hussein Shah alipotembelea
ofisi za Mamlaka hayo, Kigamboni, Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe
Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa
Meneja wa Ukaguzi wa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA-Bw.
Beatus Nchota (kulia) wakati Dkt. Mpango alipotefanya ziara ya
kushitukiza katika Ofisi za TRA-Kigamboni, Jijini Dar es Salaam kujionea
utendaji kazi wa Mamlaka hayo wakati wananchi wakijitokeza kwa wingi
kulipa kodi ya majengo. Katikati ni Afisa wa (TRA) Bw. Theraphin
Mbwambo.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe
Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akiwapongeza na kuwashukuru wananchi wa
Kigamboni waliojitokeza kulipa kodi ya majengo na kutoa rai kwa
wananchi kujenga utamaduni wa kulipa kodi kwa hiari ili kufikia uchumi
wa viwanda na kuendesha huduma za jamii.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.
Philip Mpango (Mb), akimsikiliza Msimamizi wa Kituo cha Mafuta cha
Mjimwema, Kigamboni Jijini Dar es Salaam, Bw. Yusuph Abbass baada ya
kufanya ziara ya kushitukiza katika kituo hicho na kubaini kuwa mashine
za kielektroniki za kutolea risiti hazitumiki.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.
Philip Mpango (Mb), akimsikiliza Msimamizi wa Kituo cha Mafuta cha
Mjimwema, Kigamboni Jijini Dar es Salaam, Bw. Yusuph Abbass baada ya
kufanya ziara ya kushitukiza katika kituo hicho na kubaini kuwa mashine
za kielektroniki za kutolea risiti hazitumiki.
…………………………………………………………………………………
Benny Mwaipaja, WFM-Dar es Salaam
Wakazi wa Kigamboni mkoani Dar es
Salaam, wameiopongeza Serikali kwa kusimamia vizuri masuala ya kodi na
kwamba wako tayari kuiunga mkono Serikali kwa kulipa kodi kwa hiari ili
iweze kutimiza malengo yake ya kuwahudmia wananchi kimaendeleo.
Wametoa kauli hiyo wakati Waziri
wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, alipofanya ziara ya kushitukiza
kwenye Ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, Kigamboni, ili kujionea
zoezi la wakazi wa Mji huo wanavyolipa kodi ya majengo na kutembelea
baadhi ya vituo vya mafuta ili kuona kama wamiliki wanatoa risiti
ipasavyo kwa wateja wao.
Wakitoa maoni yao kuhusu zoezi
hilo la kulipa kodi ya majengo, wakazi hao wameelezea kuridhishwa na
huduma wanayopata kutoka kwa wafanyakazi wa TRA na kuiomba Serikali
iangalie namna ya kuongeza muda wa kulipa kodi hiyo kutokana na mwamko
mkubwa uliopo hali inayoonesha kuwa huenda baadhi yao wasikamilishe
zoezi hilo ifikapo Julai 15 Mwaka huu.
“Ninampongeza sana Mhe. Rais kwa
kutupatia Waziri huyu (Dkt. Mpango), anajibu vizuri na kwa kuamua
kututembelea, pia wafanyanyakazi wa TRA wanatuhudumia vizuri sana,
tunakushukuru Mhe. Waziri” alisema kwa furaha Bi. Mary Laizer, Mkazi wa
Kigamboni
Akizungumza na wakazi hao, Dkt.
Philip Mpango amewafikishia watanzania salaam na pongezi za Mheshimiwa
Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa namna walivyoitikia wito wa kulipa
kodi na kwamba hatua hiyo itaiwezesha Serikali kuboresha huduma za jamii
kama afya, elimu, maji na miundombinu mbalimbali kutokana na mapato ya
kodi hizo
“Mkiona barabara zinajengwa,
tunafanya jitihada kuongeza dawa hospitalini, kulipa wanajeshi wetu ili
watulinde usiku wakati sisi tumelala, inatokana na nguvu tunayoipta
kutoka kwenu kupitia kodi” alisisitiza Dkt. Mpango.
Alisema kuwa amekwenda Kigamboni
kuwashukuru wakazi wa Mji huo kwa mwitikio wao mkubwa wa kulipa kodi
hususan ya majengo kwa hiari na kuangalia changamoto zinazokabili zoezi
la ukusanyaji kodi ikiwemo msongamano mkubwa wa watu na kugundua uhaba
wa baadhi ya vitendeakazi kama vile kompyuta na watumishi
Kwa upande wake Meneja Ukaguzi wa
Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Beatus Nchota, alitoa
wito kwa Watanzania kuendeleza moyo huo wa kulipa kodi kwa hiari hata
kwenye kodi nyingine za biashara ili Serikali iweze kupata mapato ya
kutosha ya kuwahudumia wananchi wake.
Wakati huo huo Waziri wa Fedha na
Mipango Dkt. Philip Mpango, ameamuru kufungwa kwa kituo cha Mafuta cha
Mawenzi kilichoko Kigamboni hadi mmiliki wake atakaporekebisha kasoro
baada ya kubaini kuwa mashine maalumu za Kieletroniki zilizofungwa
kwenye pampu za mafuta kwa ajili ya kutolea risiti hazitumiki, jambo
ambalo ni kinyume cha sheria.
Akiwa katika kituo hicho cha
mafuta, Dkt. Mpango alishuhudia mashine mbili za kielekroniki zikiwa
hazifanyikazi badala yake wahudumu wanatumia mashine za kieletroniki za
kawaida ambazo haziwezi kupima kiwango cha mafuta kinachotoka kwenye
pampu za mafuta hatua mabayo inaikosesha serikali mapato yake halisi.
Msimamizi wa Kituo hicho Bw.
Yusuph Abbass alisema kuwa mashine hizo zote mbili zilipata hitilafu
juma moja lililopita na kulazimika kutumia mashine za EFD za kawaida
jambo ambalo lilipingwa na Waziri Dkt. Mpango kwa kuwa ni kinyume cha
taratibu na sheria na maelekezo ya Serikali.
Kufuatia hatua hiyo Dkt. Mpango
ameiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuvikagua na kuvifunga vituo
vyote vya mafuta nchini ambavyo havijafunga machine hizo za kutolea
risiti kama wamiliki wake walivyoagizwa na Serikali tangu mwaka jana
hatua ambayo inaikosesha Serikali mapato yake.
SHARE
No comments:
Post a Comment