Waziri Ummy akimsalimia mtoto
aliyefika kituoni na mama yake kupata huduma ya afya, Waziri huyo
amefika katika kituo hicho ili kujionea hali ya kituo hicho ambacho
kinahudumia idadi kubwa ya wakazi wa mji huo pamoja na jirani zake licha
ya kuwa na changamoto ya watumishi pamoja na miundombinu ili
kuwezesha vituo vya afya nchini kote vinafikia malengo ya serikali
katika kuboresha afya na huduma za afya kwa watanzania.
Moja ya Vipaumbele vya Serikali
ya Awamu ya Tano ni Upatikanaji wa Dawa kwenye vituo vyote vya
Serikali,Waziri Ummy Mwalimu akiongea na watoa huduma kwenye dirisha la
dawa katika kituo hicho.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto akimfafanulia jambo mmoja wa wagonjwa
waliofika kupata huduma kwenye kituo cha afya cha Katoro
Waziri Ummy akitoa maelekezo
kwenye matangazo yaliyobandikwa kwenye kuta za kituo hicho,kushoto ni
Mkurugenzi wa HALMASHAURI YA Geita Lawrence Kalabezile.Waziri huyo
amewataka watumishi wa kituo hicho kujituma na kutimiza wajibu wao
katika kuwahudumia wananchi hususan katika kuokoa maisha ya wagonjwa.
Katika ziara hivyo Waziri Ummy
alikagua ujenzi wa jengo la upasuaji wa dharura unaojengwa kwenye kituo
hicho.Waziri wa Afya yupo katika ziara ya kikazi ya siku tatu Mkoani
Geita (PICHA ZOTE NA WIZARA YA AFYA)
SHARE
No comments:
Post a Comment