WAZIRI wa Fedha na Mipango,
Mhe Dkt. Philip Mpango ametaka kuwapo na uratibu wenye maslahi mapana
katika biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China.
Alisema hayo wakati akifungua mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China.
Alisema mahusiano yaliyopo kati
ya Tanzania na China ambayo ni ya kihistoria yasitumike vibaya bali
yanahitaji kuratibiwa kiuangalifu kwa maslahi ya pande zote mbili.
Aliwataka washiriki wa mkutano
huo wa mwaka kujadili kwa makini namna ya kuratibu vizuri vitega uchumi
na biashara kwa manufaa ya nchi zote mbili.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe Dkt. Philip Mpango akisoma hotuba kwa niaba ya
Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) wakati
akifungua mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na
uwekezaji kati ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Alielezea kufurahishwa kuwapo na
mada mbalimbali zinaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na
China na kusema mada hizo zitumike vyema kuweka misingi mizuri yenye
manufaa kwa pande zote mbili.
Aidha aliipongeza ESRF kwa kuona
haja ya kuwapo kwa mazungumzo ya aina hiyo na kusema kupitia tafiti
mbalimbali taifa hili litaenda mbele katika kujenga uchumi wa viwanda.
Mkutano huo unaohusisha washiriki
mbalimbali wa ngazi za juu wa biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na
China umeitwa kama sehemu ya mchango wa ESRF katika ujenzi wa uchumi wa
viwanda wa Tanzania.
“Sisi serikalini
tunaridhishwa na juhudi zinazofanywa na taasisi za kitafiti kama hii
zenye lengo la kusaidia juhudi za serikali za kuhudumia watu wake na
kuongeza ustawi” alisema Mpango.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi
Kida akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki wa mkutano wa 6 wa mwaka wa
ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China
uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo ambao unazungumzia
mahusiano ya kibiashara na uwekezaji umeelezwa na Mh. Dk Mpango kuwa
moja ya mikutano inayotoa fursa za kuangalia uwekezaji wenye tija
unaozingatia maslahi mapana ya mataifa husika.
Alisema Tanzania na China zina
uhusiano mzuri wa kihistoria na hadi sasa na kwamba kinachostahili ni
kuoanisha uhusiano huo na kuuweka katika hali bora zaidi za kunufaisha
pande zote mbili.
Baadhi ya miradi mikubwa ambayo
Tanzania imesaidiwa na China ni pamoja na ujenzi wa Reli ya Tanzania na
Zambia (TAZARA) na kiwanda cha Urafiki; kuanzishwa kwa shamba la mpunga
la Mbarali; kiwanda cha sukari cha Mahonda na mgodi wa mawe wa Kiwira.
Mwenyekiti
wa bodi ya ESRF, Philemon Luhanjo akizungumza machache kabla ya
kumkaribisha mgeni rasmi kufungua mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF
unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China
uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Kwa sasa China ni moja ya taifa
lililo na uwekezaji mkubwa nchini Tanzania pia ikifanya shughuli nyingi
za ujenzi zenye gharama kubwa kama daraja la Kigamboni na barabara.
Naye Mwenyekiti wa bodi ya ESRF,
Philemon Luhanjo, akimkaribisha Mheshimiwa Waziri Mpango alisema kwamba
alisema kwamba mkutano huo umeandaliwa kwa pamoja kati ya ESRF na Chuo
kikuu cha Kilimo cha China.
Alisema mkutano huo umewaleta
pamoja wanazuoni wa Kichina na Kitanzania kuangalia mahusiano yaliyopo
na kutengeneza mustakabli bora wa namna ya kushirikiana.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa
Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida amesema
kwamba mkutano huo ni sehemu ya juhudi za kusaidia serikali kwa njia ya
utafiti ambapo majibu yanatumiwa kutengeneza sera au majibu ya
changamoto mbalimbali.
Mkutano huo ulifungwa na Waziri Mkuu mstaafu, Mh. Dkt. Salim Ahmed Salim.
Mwakilishi
wa Ubalozi wa China nchini Tanzania anayeshughulikia wa Masuala ya
Uchumi na Biashara, Lin Zhiyong akizungumza kwa niaba ya balozi wa China
wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia
biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar
es Salaam. Katibu
Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Profesa Adolf Mkenda
akiwasilisha mada inayohusu namna watanzania wanavyoweza kunufaika na
fursa za kibiashara na uwekezaji China wakati wa mkutano wa 6 wa mwaka
wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China
uliofanyika jijini Dar es Salaam. Pichani
juu na chini ni sehemu ya washiriki kutoka China na Tanzania
waliohudhuria mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na
uwekezaji kati ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
ya Taasisi ya Utafiti wa Maendeleo China (CIDRN), Prof. Dr. Li Xiaoyun
akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki wa mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF
unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China
uliofanyika jijini Dar es Salaam. Balozi
wa Tanzania nchini China, Mh. Mbelwa Kairuki akizungumzia namna ambavyo
watanzania wanaweza wakafaidika na fursa za biashara na uwekezaji
nchini China wakati wa mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia
biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar
es Salaam. Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka akiwasilisha mada inayohusu mahusiano
ya kibiashara ya uwekezaji kati ya Tanzania na China kwa mtazamo wa
Serikali za Mitaa wakati wa mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia
biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar
es Salaam. Kutoka
kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii
(ESRF), Dk. Tausi Kida, Balozi wa Tanzania nchini China, Mh. Mbelwa
Kairuki, Waziri Mkuu mstaafu, Dkt. Salim Ahmed Salim, Mwenyekiti wa bodi
ya ESRF, Philemon Luhanjo, Mwenyekiti na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni
za Infotech Investment, Ali Mfuruki wakifuatilia mada mbalimbali
zilizokuwa zikiwasilisha wakati wa mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF
unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China
uliofanyika jijini Dar es Salaam. Mkutano ukiendelea. Balozi
wa Tanzania nchini China, Mh. Mbelwa Kairuki pamoja na Waziri Mkuu
mstaafu, Dkt. Salim Ahmed Salim wakifuatilia mada mbalimbali zilizokua
zikiwasilishwa katika mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia
biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar
es Salaam. Profesa
Humphrey Moshi kutoka idara ya Uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam akiwasilisha mada inayohusu uhusiano wa China na Tanzania katika
masuala ya uwekezaji na biashara wakati wa mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF
unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China
uliofanyika jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka Maalum ya Uwekezaji (EPZA), Kanali Mstaafu Joseph
Simbakalia akichangia maoni wakati wa mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF
unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China
uliofanyika jijini Dar es Salaam. Mwanachama
wa Chama cha Wanafunzi walisomea China (CAAT), Linas Kahisha akielezea
uzoefu wake katika fursa za kibiashara nchini humo katika mkutano wa 6
wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na
China uliofanyika jijini Dar es Salaam. Pichani
juu na chini ni washiriki kutoka Tanzania na Chini waliohudhuria
mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati
ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mgeni
rasmi Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe Dkt. Philip Mpango, Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida
na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka wakiwa katika picha ya pamoja
na wanafunzi watafiiti kutoka nchini China. Mkuu
wa Idara ya Utafiti na Machapisho wa ESRF, Prof. Fortunata Makene
(kushoto) katika picha ya kumbukumbu na Mkuu wa Idara ya Maarifa na
Ubunifu wa ESRF, Bi. Margareth Nzuki (kulia) mara baada ya ufunguzi
rasmi wa mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na
uwekezaji kati ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi
Kida (katikati), Mkuu wa Idara ya Maarifa na Ubunifu wa ESRF, Bi.
Margareth Nzuki na Mwenyekiti ya Taasisi ya Utafiti wa Maendeleo China
(CIDRN), Prof. Dr. Li Xiaoyun katika picha ya kumbukumbu. Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka (katikati) katika picha ya pamoja na
washiriki kutoka TPSF na ESRF na Mshereshaji wa mkutano huo Eng. George
Mulamula (kushoto). Baadhi
ya washiriki kutoka China wakichukua baadhi ya makabrasha yenye taarifa
mbalimbali zilizoandaliwa na ESRF wakati wa mkutano wa 6 wa mwaka wa
ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China
uliofanyika jijini Dar es Salaam. Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe Dkt. Philip Mpango akisalimiana na Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida
alipowasili katika ufunguzi wa mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF
unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China
uliofanyika jijini Dar es Salaam. Mgeni
rasmi Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe Dkt. Philip Mpango (katikati)
akiongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na
Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida (kushoto) na Mwenyekiti wa bodi ya ESRF,
Philemon Luhanjo baada ya kuwasili katika mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF
unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China
uliofanyika jijini Dar es Salaam. Mgeni
rasmi Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe Dkt. Philip Mpango katika picha
ya kumbukumbu na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na
Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida mara baada ya kufungua mkutano wa 6 wa
mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na
China uliofanyika jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment