WATANZANIA wameshauriwa kuchangamkia
fursa za ufugaji wa samaki kibiashara kutokana na kuwepo kwa soko kubwa
la bidhaa hiyo huku mnyororo wake wa thamani ukiwa na uhai mrefu
kisekta.
Kauli hiyo imetolewa na Ofisa wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa
Mataifa (UNDP) Bwana Amon Manyama wakati akifunga warsha ya siku moja
juu ya ufugaji wa samaki kibiashara iliyofanyika katika viwanja vya
Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) mwishoni mwa wiki na
kuhudhuriwa na watu takribani 400.
Bw. Manyama alisema kwamba watanzania wasipotumia fursa ya ufugaji wa
samaki baada ya miaka mitano watakuwa wamepoteza fursa hiyo adimu
inayoshawishi viwanda vidogo na vya kati. Alisema kimsingi yeye anaamini
sekta ya ufugaji wa samaki ni viwanda tosha kutokana na muingiliano
wake huku watu wakinufaika na minofu pia kuna ngozi na magamba ambayo
yanakazi kubwa ya kutengeneza urembo, viatu na kadhalika. Mkuu
wa Idara ya Maarifa na Ubunifu ya Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na
Kijamii (ESRF), Margareth Nzuki akitambulisha wageni na malengo ya
warsha ya fursa za ufugaji Samaki kibiashara.[/caption]
Warsha hiyo imeandaliwa na Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii
(ESRF)- Kitengo cha Maarifa na Ubunifu ikishirikiana na Chuo Kikuu cha
Kilimo cha Sokoine (SUA)- Idara ya Sayansi ya Wanyama, Ukuzaji Viumbe
Majina Nyanda za Malisho, Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) - Kikosi cha
Kambi la Rwamkoma pamoja na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa
(UNDP) ilifunguliwa na Bi. Ritha Maly Kaimu Mkurugenzi Idara ya
maendeleo ya viumbe wa majini.
Akifungua warsha hiyo, Bi Ritha aliwashukuru waandaaji wa warsha hii kwa
sababu ya uhitaji mkubwa wa samaki "Warsha hii imekuja wakati
muafaka ambapo uhitaji wa samaki umeongezeka sana ukiambatana na
changamoto za upatikanaji wa samaki wa kutosha hivyo uwepo wa fursa
hizi zitakazowasilishwa leo zitakua hakika ni mkombozi mkubwa kwa kukuza
uzalishaji wa samaki nchini na kufungua fursa za biashara ya samaki kwa
kufanya ufugaji huu kibiashara." alisema. Makamu
Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Viumbe Hai Majini wa Wizara ya Kilimo,
Mifugo na Uvuvi, Ritha Maly akisoma hotuba ya kufungua warsha ya fursa
za ufugaji samaki kibiashara.[/caption]
Akielezea madhumuni na lengo la kufanya washa hii, Mkuu wa Kitengo cha
Maarifa na Ubunifu (ESRF) Bi. Margareth Nzuki, alisema warsha hii ni
mwendelezo wa warsha nyingine ambazo zinalenga kuwaelimisha wananchi
fursa zilizopo katika sekta ya kilimo na uvuvi ambazo tukitumia teknojia
za kisasa zinaweza kuongeza kipato na kujenga uchumi,
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF Dkt. Tausi Kida akimkaribisha mgeni
rasmi kuzungumza na watu mbalimbali waliojitokeza katika mafunzo hayo
wakiwamo wafugaji na wanaotaka kuanza kufuga, alisema amefurahishwa na
mahudhurio na kusema ameona ishara kubwa ya dhamira ya kufanya mapinduzi
makubwa katika eneo la ufugaji wa samaki kwa kuwa tayari kutafuta
maarifa juu ya ufugaji samaki kibiashara. Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi
Kida akisoma hotuba ya ukaribisho katika warsha ya fursa za ufugaji
samaki kibiashara.[/caption]
Alisema Taasisi ya ESRF baada ya kufanya utafiti na kuwa na matokeo
iliamua kuitisha warsha hiyo ili kwa mara nyingine tena kuopeleka faida
ya kivitendo kwa wananchi ili waweze kujikwamua kiuchumi na kusukuma
mbele gudurumu la maendeleo.
"Taasisi yetu imekuwa msitari wa mbele kufanya tafiti mbali mbali ambazo
kwa hakika zimekuwa na faida na matokeo makubwa kwa maendeleo ya jamii
na taifa kwa ujumla. Kufuatia tafiti mbalimbali, msukumo na muitikio
mkubwa wa jamii umeonekana katika maeneo mbali mbali ikiwemo pia ufugaji
wa samaki." alisema Dkt. Kida na kuongeza kuwa Taasisi hiyo kwa
kushirikiana na wadau mbali mbali imefanya tafiti juu ya fursa mbali
mbali zinazoweza kutokea kutokana na ufugaji samaki. " Afisa
Mifugo wa Kituo cha Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi cha Bagamoyo,
Emmanuel Maneno akitoa wasilisho la kwanza kuhusu Ufugaji wa Samaki
katika Mabwawa.[/caption]
Warsha hii ilikuwa na mada mbalimbali ambazo ziliwakilishwa na wataalam
waliobobea katika sekta ya ufugaji wa samaki. Katika mada mbalimbali
washiriki walisisitizwa kuwa makini na kutohemka na kuhakikisha kwamba
wanwatumia wataalamu hasa kupata mafunzo kabla ya kuingia katika
shughuli za ufugaji.
Akizungumzia ufugaji wa samaki katika mabwawa (pond fish farming),Bwana
Emmanuel Maneno wa Kituo Cha Ufugaji Samaki Mbegani - Idara Ya Ukuzaji
Viumbe Majini, alisema kwamba wataalamu wa serikali na wale wa
halmashauri hufanyakazi ya upembuzi wa maeneo bure suala ni kuwafikisha
katika eneo huisika ili aweze kuangalia eneo na kukushauri aina ya
bwawa. Mkurugenzi
wa Nuru Farm, Gloria Kavisheakitoa wasilisho kutoka kwa mfugaji kuhusu
Ufugaji wa Samaki katika Mabwawa.[/caption]
Aidha mmoja wa wafugaji anayefanya ufugaji kibiashara kwa ufugaji mkubwa
(large scale) kutoka Ruvu Farm, Bwana Nkhumbo Kantenga alizungumzia
changamoto mbalimbali ambazo wanakabiliana nazo katika ufugaji wa
kibiashara lakini akisema kwamba kila changamoto inatolewa ufumbuzi na
kwamba shamba lake linauza pia vifaranga na vyakula vya kuku. Pia Bi.
Gloria Kavishe wa Nuru Farm mfugaji mdogo (small scale) alitoa uzoefu
wake katika ufugaji wa samaki kibiahsara akihimiza watu wajiunge na
biashara ya samaki kwa kuwa inalipa.
Katika mada ya ufugaji katika vizimba mada ilitolewa na Luteni Kelvin
Ngondo kutoka Jeshi la Kujenga Taifa – Kambi ya Rwamkoma, ufugaji huu
unaonekana zaidi katika maeneo ya bahari na maziwa kwa kuwa unafaida
nyingi mfano mfugaji kama atawafuga samaki wake kwa kufuata kanuni zote
za ufugaji ana hakika ya kuwavuna samaki wengi wenye viwango bora.
Kizimba kimoja kinaweza kuchukua samaki hadi elfu 5. Pia husaidia
kuwaondoa uvuvi haramu lakini pia unatoa uwapo wa makundi ya ushirika
ambayo yanaweza kusaidia kupata nafuu katika ulinzi na pia katika uwingi
wa idadi ya samaki. Meneja
wa Ruvu Farm, Nkhumbo Kantenga akitoa wasilisho kutoka kwa mfugaji
mkubwa kuhusu Ufugaji wa Samaki katika Mabwawa.[/caption]
Mtaalamu kutoka SUA Dkt. Nazael Madalla alizungumzia kwa undani namna
ya kulisha samaki, uandaaji wa vyakula vyake na pia kujibu maswala
muhimu kuhusu magonjwa na mana bora ya kupunguza gharama za chakula ili
kuweka faida juu.
Dkt. Gratian Bamwenda, Mtafiti Mshiriki wa ESRF, alitoa mada iliyohusu
muingiliano wa ufugaji wa samaki kibiashara na masoko ya samaki. Alisema
utunzaji na uhifadhi mzuri wa samaki baada ya kuvuliwa unasaidia sana
kupata soko zuri la bidhaa hiyo. Alitoa mifano mbalimbali ya kutunza
samaki ili kumsaidia mfugaji wa samaki kupata soko la uhakika. Luteni
Kelvin Ngondo kutoka kikosi cha Jeshi la Wananchi 822 Rwamkoma cha
Butiama, Mara akiwasilisha akitoa wasilisho kuhusu ufugaji wa samaki
katika vizimba.[/caption]
Licha ya mada mbalimbali za kuelimisha zilizotolewa na wakufunzi,
washiriki walipata nafasi kumsikiliza Ofisa kutoka Benki ya Maendeleo
ya Kilimo Bwana Marko Samson ambaye aliwahakikishia washiriki wa warsha
kwamba benki hiyo ipo wazi kwa elimu na pia kwa kupata mitaji.
Pamoja na wananchi zaidi ya 400 kufika kutafuta utaalamu wa namna ya
kufuga huku wakioneshwa video, pia wanawarsha walipewa angalizo la
utafutaji wa masoko ya uhakika kabla ya ufugaji kwani ni hatari kuanza
kufuga ukiwa hujui soko liko wapi. Afisa Uvuvi wa Samaki kutoka SUMA JKT, Luteni Joseph Lyakurwa akitoa wasilisho la ufugaji samaki katika matanki. Mkuu
wa Idara ya Sayansi ya Wanyama, Ukuzaji viumbe maji na Nyanda za
malisho wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Dk. Nazael Madalla. Mtafiti Mwenza wa ESRF, Dk. Gratian Bamwenda akitoa wasilisho kuhusu masoko ya bidhaa za samaki. Afisa
Mwandamizi anayeshughulikia na kuendeleza wakulima wadogo wa Benki ya
Maendeleo ya Kilimo (TADB), Marco Samson akieleza jinsi benki hiyo
inavyowasaidia wakulima na wafugaji wadogo kukuza biashara zao. Mkuu
wa Programu, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP, Amon
Manyama akifunga warsha ya fursa za ufugaji samaki kibiashara. Mkurugenzi
Mtendaji wa ESRF, Dk. Tausi Kida na Mkuu wa Idara ya Maarifa na Ubunifu
ya ESRF, Margareth Nzuki wakimpa maelezo mgeni rasmi kwenye warsha ya
fursa za ufugaji samaki kibiashara, Makamu Mkurugenzi wa Idara ya
Ukuzaji Viumbe Hai Majini wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Ritha
Maly kuhusu ufugaji samaki wa kwenye matanki. Baadhi ya washiriki wa warsha ya fursa za ufugaji samaki kibiashara wakipewa maelezo kuhusu ufugaji samaki wa kwenye matanki. Picha juu na chini ni Baadhi ya washiriki wa warsha ya fursa za ufugaji samaki kibiashara.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi
Kida akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Programu, Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP, Amon Manyama na Mkuu wa Idara ya
Maarifa na Ubunifu ya Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF),
Margareth Nzuki.
SHARE
No comments:
Post a Comment