Mke
wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majalwa akizungumza na wanafujnzi wa Shule ya
Sekondari ya Vwawa iliyop[o Mbozi baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
kuzungumza na watumishi wa umma, viongozi wa dini na viongozi wa taasisi za
binafsi kwenye ukumbi wa shule hiyo Julai 23, 2017 . (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
NA
OWM, VWAWA
MKE wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa amewasihi wanafunzi wa
kike nchini kujiepusha na vitendo vinavyoweza kusababisha kukatisha masomo yao.
Amesema ni vema wanafunzi hao wakatumia muda wao vizuri kwa
kusoma kwa mfululizo kutoka kiwango kimoja cha taaluma kwenda kingine.
Mama Mary aliyasema hayo jana (Jumapili, Julai 23, 2017)
alipozungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Vwawa wilayani Mbozi.
Mke wa Waziri Mkuu ambaye ameambatana na Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa katika ziara ya mkoa Songwe, aliwaasa wanafunzi hao kutumia wakati huu
kwa kusoma kwa bidii na kujiepusha na vitendo viovu.
“Nawasihi mtumie muda huu kusoma kwa bidii ili muweke msingi
imara kwa ajili ya kujenga maisha yenu ya baadae. Msikatishe masomo yenu.”
Mama Mary aliongeza kwamba “utumieni muda huu vizuri ili msije
mkaujutia baadae, kwani wakati ni mali ukipita umepita.”
Alisema ni vizuri wakasoma hadi chuo kikuu na kwamba
wasikimbilie kufanya mambo yasiyowahusu kwa sasa kwani mshika mawili moja
lazima limponyoke.
Mke wa Waziri Mkuu alisema wanafunzi hao wakisoma hadi elimu ya
juu watakuwa na uwezo wa kutambua jambo lipi ni jema na lipi ni baya.
“Kilichonifurahisha zaidi ni kwa sababu mimi pia ni mwalimu kwa
hiyo inavyoona wanafunzi wako vizuri kama hivi nafurahi sana, hivyo nawaomba
msome kwa bidii.”
Serikali imetunga sheria kali dhidi ya watu wanaosababisha
watoto wa kike kukatisha masomo yao kwa kuwapa mimba au kuwaoa.
SHARE
No comments:
Post a Comment