Mkurugenzi
Mtendaji wa Huawei Tanzania, Gao
Mengdong akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya uzinduzi wa programu ya ‘Seeds
for the future’ kwa mwaka 2017 inayoratibiwa na Kampuni hiyo kila mwaka jijini Dodoma. Programu hiyo ni mwendelezo wa dhamira ya kampuni hiyo katika
kupanua wigo wa ushirikiano na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ambapo
kwa kushirikiana na Wizara, Huawei huchukua wanafunzi 10 wa vyuo vikuu kila
mwaka wanaochukua masomo ya TEHAMA na kuwapeleka nchini China kwenda kujifunza
kwa vitendo ili kuongeza uwezo kwenye masuala ya TEHAMA.
Mkurugenzi wa Idara ya
Elimu ya Juu, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Prof. Sylvia Temu akizungumza
wakati wa hafla ya uzinduzi wa programu
ya ‘Seeds for the future’ iliyozinduliwa na Kampuni ya Huawei kwa mwaka 2017 jijini
Dodoma jana. Programu hiyo ni mwendelezo wa dhamira ya kampuni hiyo katika
kupanua wigo wa ushirikiano na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ambapo
kwa kushirikiana na Wizara, Huawei huchukua wanafunzi 10 wa vyuo vikuu kila
mwaka wanaochukua masomo ya TEHAMA na kuwapeleka nchini China kwenda kujifunza
kwa vitendo ili kuongeza uwezo kwenye masuala ya TEHAMA.
Mkurugenzi wa kitengo
cha TEHAMA wa chuo Kikuu Dodoma Dkt. Hector Mongi akizungumza wakati wa hafla
ya uzinduzi wa programu ya ‘Seeds for the future’ iliyozinduliwa
na Kampuni ya Huawei jijini Dodoma leo. Programu hiyo ni mwendelezo
wa dhamira ya kampuni hiyo katika kupanua wigo wa ushirikiano na Wizara ya
Elimu, Sayansi na Teknolojia ambapo kwa kushirikiana na Wizara, Huawei huchukua
wanafunzi 10 wa vyuo vikuu kila mwaka wanaochukua masomo ya TEHAMA na
kuwapeleka nchini China kwenda kujifunza kwa vitendo ili kuongeza uwezo kwenye
masuala ya TEHAMA.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo (wa pili
kulia) akizungumza
wakati wa hafla ya uzinduzi
wa programu ya ‘Seeds for the future’ iliyozinduliwa na Kampuni ya Huawei jijini
Dodoma leo. Programu hiyo ni mwendelezo wa dhamira ya kampuni hiyo katika
kupanua wigo wa ushirikiano na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ambapo
kwa kushirikiana na Wizara, Huawei huchukua wanafunzi 10 wa vyuo vikuu kila
mwaka wanaochukua masomo ya TEHAMA na kuwapeleka nchini China kwenda kujifunza
kwa vitendo ili kuongeza uwezo kwenye masuala ya TEHAMA.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo (kulia) na
Mkurugenzi wa Huawei Tanzania, Gao
Mengdong wakitia saini kwenye mkataba wa makubaliano wa kushirikiana
katika programu ya ‘Seeds for the future’ wakati wa hafla ya uzinduzi wa programu hiyo iliyozinduliwa
na Kampuni ya Huawei jijini Dodoma jana. Programu hiyo ni mwendelezo wa dhamira
ya kampuni hiyo katika kupanua wigo wa ushirikiano na Wizara ya Elimu, Sayansi
na Teknolojia ambapo kwa kushirikiana na Wizara, Huawei huchukua wanafunzi 10
wa vyuo vikuu kila mwaka wanaochukua masomo ya TEHAMA na kuwapeleka nchini
China kwenda kujifunza kwa vitendo ili kuongeza uwezo kwenye masuala ya TEHAMA.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo (kulia) na
Mkurugenzi wa Huawei Tanzania, Gao
Mengdong wakipeana mkono baada ya kutia saini kwenye mkataba wa
makubaliano wa kushirikiana wakati wa uzinduzi wa programu ya ‘Seeds for the
future’ iliyozinduliwa na Kampuni
ya Huawei jijini Dodoma jana. Programu hiyo ni mwendelezo wa dhamira ya
kampuni hiyo katika kupanua wigo wa ushirikiano na Wizara ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia ambapo kwa kushirikiana na Wizara, Huawei huchukua wanafunzi 10 wa
vyuo vikuu kila mwaka wanaochukua masomo ya TEHAMA na kuwapeleka nchini China
kwenda kujifunza kwa vitendo ili kuongeza uwezo kwenye masuala ya TEHAMA.
Picha ya pamoja
Dodoma, 25 Julai, 2017: Katika kuchangia maendeleo ya elimu nchini
Tanzania, Kampuni ya Huawei inayoongoza ulimwenguni katika utoaji wa huduma ya
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) leo imeendeleza juhudi zake kwa
kusaidia sekta ya elimu nchini Tanzania kwa kuzindua programu yake ya kila
mwaka ya ‘Seeds for the future’.
Uzinduzi wa
programu hiyo umefanyika leo katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM). Huawei
imeeleza dhamira yake ya dhati katika kupanua wigo wa ushirikiano na Wizara ya
Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Mafunzo ya Ufundi katika kupanua maarifa
ya masomo ya TEHAMA kwa wanafunzi na watendaji wanaofanya kazi kwenye sekta ya
Mawasiliano na Teknolojia.
Akizungumza katika
hafla ya uzinduzi huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dkt.
Leonard Akwilapo, alipongeza juhudi za Huawei katika kuibua vipaji kwenye sekta
ya TEHAMA nchini Tanzania na kushirikiana kikamilifu na wananchi.
Dkt. Akwilapo alimwakilisha
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.
Joyce Ndalichako ambao walitarajiwa kuzindua programu hiyo ya TEHAMA.
Dkt. Akwalipo
alisema Huawei imekuwa mshirika muhimu waTanzania katika kukuza maendeleo ya TEHAMA
nchini na imeendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika uvumbuzi wa masuala
hayo kutokana na Serikali kuendelea kuboresha Teknolojia kupitia miradi yake
mbalimbali.
“Ninapenda
kuwashukuru Huawei kwa kile walichokianzisha na kuendeleza Programu ya ‘Seeds
for the Future’ kwa wanafunzi wa Tanzania. Ninawahakikisha kwamba Wizara ya
Elimu itaendelea kushirikiana na Huawei kwa sababu tunatambua kwamba TEHAMA ni
muhimu sana pia katika kusaidia maendeleo ya elimu,”
Aliongeza kuwa Programu
ya Seeds for the Future inaendeshwa na Huawei ulimwenguni kote kupitia kitengo
chake cha Corporate Social Responsibility (CSR). Kupitia programu hii Huawei
Tanzania imejiwekea mikakati ya kuhakikisha wanafunzi 100 kutoka hapa nchini
wanashiriki katika mradi wa miaka 10 ambapo inamaanisha kwamba kila mwaka
wanafunzi 10 kutoka hapa nchini watapata fursa ya kutembelea Beijing na kufanya
kazi na kampuni hii katika makao makuu yake yaliyopo Shenzhen, China.
Katika tukio hilo,
Huawei pia ilisaini mkataba na Wizara ya Elimu kuhusu utekelezaji wa kukuza
vipaji katika kuendeleza ICT unaojulikana ‘Huawei ICT Talent Cultivation Plan’
ambapo utawanufaisha vijana wenye taaluma, maofisa wa serikali na wahadhiri.
Malengo ya mpango
huo ni kutekeleza programu ya kuhamasisha elimu ya TEHAMA iliyolenga kuinua
kiwango cha elimu na kuendeleza mafunzo kwa wanafunzi wanaosoma ICT. Hususani
kukuza ushirikiano na Huawei ambao utaendeleza vituo vya mafunzo na kuanzisha
madarasa maalumu katika ofisi za Huawei Tanzania.
Kupitia mkataba
huo wa makubaliano uliosainiwa leo, tutaimarisha vituo vya kitaaluma katika
ofisi za Huawei, Huawei Tanzania Customer Solution Intergration &
Innovation Experience Centre (CSIC) na madarasa.
Zaidi ya hayo tutatoa nafasi
za mafunzo kwa wanafunzi wa ICT kufanya kazi za muda katika ofisi za Huawei
Tanzania jambo ambalo litawasaidia kujifunza, kufanya tafiti na kuendelea ujuzi
wao kwenye masuala ya TEHAMA,” alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Huawei Tanzania,
Bwana Gao Mengdong.
Aidha, Huawei pia
imedhamiria kutimiza ahadi yake ya kupanua ushirikiano wake na serikali katika
kuanzisha mradi wa mafunzo kwa matandao ambao ushirikiano huo utatoa mchango
mkubwa zaidi kwa sekta ya elimu nchini Tanzania na maendeleo ya ICT ili
kuifanya Tanzania kufikia malengo ya dira ya maendeleo ya mwaka 2025.
Kwa mujibu wa
Gao, falsafa ya Huawei ni ‘Expoloration’ ikiwa na maana kwamba kampuni
itaendelea kubuni kila namna ili kuiwezesha nchi kuendelea kutimiza mipango
yake ya maendeleo.
Miongoni mwa
wanafunzi walioteuliwa kushiriki programu hii, Kadhija Mohammed aliipongeza
Huawei kwa kuendelea kuibua vipaji vya ICT nchini Tanzania na kuendelea
kushirikiana na wananchi.
Alisema Huawei
imekuwa msharika muhimu kwa maendeleo ya ICT nchini Tanzania na imeendelea
kuisaidia Serikali ya Tanzania katika uvumbuzi wa ICT ambapo serikali imekuwa
ikiendelea kuboresha ICT kupitia miradi yake mbalimbali.
“Ni matumaini
yetu kwamba Serikali ya Tanzania itatumia vyema fursa iliyotolewa na Huawei na
tunaamini kupitia Programu ya Seeds for the Future tutajifunza mambo mengi
kutoka kwa Huawei Tanzania,” alisema.
SHARE
No comments:
Post a Comment