MFUKO wa LAPF umeonesha utendaji bora katika utoaji huduma na kupata tuzo ya mshindi wa kwanza kwenye kipengele cha mifuko ya hifadhi ya jamii na bima.
Rais John Magufuli alikabidhi tuzo hiyo kwa Meneja Masoko na Uhusiano wa mfuko huo, James Mlowe kama inavyoonekana pichani.
Rais John Magufuli akikabidhi ngao ya ushindi wa kwanza, James Mlowe Meneja Masoko na Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF huku akiwa na furaha baada ya mfuko huo kupata ushindi wa kwanza kwa kampuni za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na Bima
wakati wa ufunguzi rasmi wa maonyesho ya Sabasaba yanayoendelea
kwenye viwanja vya Sabasaba Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Kulia wanaoshuhudia ni Mwenyekiti wa Bodi ya TANTRADE, Christopher Chiza na Waziri wa Viwanda , Biashara na Uwekezaji,Charles Mwijage.
Rais John Magufuli akifurahia jambo mara baada ya
kumkabidhi ngao ya ushindi wa kwanza kwa Meneja wa Masoko na Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, James Mlowe baada ya kupata ushindi wa kwanza kwa kipengele hicho. Kutoka kulia wanaoshuhudia ni Mwenyekiti wa Bodi ya TANTRADE, Christopher Chiza na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage.
SHARE
No comments:
Post a Comment