Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro.
Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro ametoa agizo kuwa mchakato
ufanyike wa kuzivunja timu zote za jeshi la polisi zinazoshiriki ligi za
soka za madaraja tofauti ili iundwe timu moja.
Kamanda Sirro amesema
kuwa hatua hiyo itachukuliwa ili kuifanya timu moja ambayo itaundwa iwe
na nguvu na kuwe na maandalizi mazuri kuliko ilivyo sasa ambapo kuna
timu nyingi lakini hazifanyi vizuri.
IGP Sirro amesema amesisitiza kuwa
ameshatoa mwongozo kwa kamishna wa idara husika ili mchakato wa kuzifuta
timu zilizopo katika madaraja tofauti ufanyike kwa faida ya kulipa
jeshi nguvu liwe na timu moja imara.
Timu hiyo ambayo itaundwa
itafahamika kwa jina la Polisi Tanzania na itakuwa inachukua wachezaji
wenye vipaji vya juu kutoka katika vituo mbalimbali vya Jeshi la Polisi.
Kuhusu michezo mingine, IGP Sirro amesema inafanyika lakini
vijana wake wanahitaji motisha ili waweze kuonekana, na kusisitiza kuwa
hilo litafanyika ili kuboresha michezo mingine ikiwemo ndondi, mieleka
na judo.
SHARE
No comments:
Post a Comment