Mwenyekiti wa halmashauri ya Mafinga Mjini Charles Makoga akizungumza wakati wa baraza la madiwani wa halmashauri hiyo
Baadhi ya madiwani wa halmashauri ya Mji wa Mafinga wakiwa katika baraza pamoja na wataalamu mbalimbali wa halmashauri hiyo.
Na fredy Mgunda, Mafinga
Halmashauri
ya Mji wa Mafinga mkoni Iringa inatarajia kukuza mapato katika mwaka
Mpya wa 2017/2018 kutokana na kuanza kuzitumia sheria mpya za ukusanyaji
mapato pamoja na kuvijua vyanzo vingine vya mapato ambavyo ndio
vitasababisha kukuza uchumi wa halmashauri hiyo.
Akizungumza
wakati wa baraza la madiwani Mwenyekiti wa halmashauri ya Mafinga Mjini
Charles Makoga alisema kuwa sheria mpya walizoletewa toka mwezi wa tano
zinawapa nafasi ya kuanza kuzitumia wakati wa kukusanya mapato katika
maeneo ambayo walikuwa hawakusanyi.
"Tulikuwa
hatukusanyi mapato katika maeneo ya stand,sehemu za maegesho ya
magari,sokoni na maeneo mengine kwa kuwa sheria zilikuwa bado si rafiki
kwetu kwenda kukusanya mapato ila kwa mwaka unaoanza tutakusanya mapato
na kukuza mapato kutoka asilimia 56 hadi kuvuka lengo la serikali la
asilimia 80" alisema Makoga
Makoga
aliwataka wananchi na viongozi kushiriana kukusanya mapato kulingana
vyanzo ambavyo madiwani wameviolozesha kwa manufaa ya halmashauri ya
Mafinga Mjini ambavyo vipo kisheria kutoka serikali kuu.
Jamani
naombeni mchango wetu kufanikisha swala hili la kukusanya mapato ili
tufikie lengo la serikali kwa kuwa mwaka huu hatufikia lengo hilo ni
aibu kubwa kwa serikali hii ya awamu ya tank ambayo inaenda kwa kasi
kubwa kwa kukuza uchumi wa nchi.
Nao
baadhi ya madiwani wa halmashauri ya mji wa mafinga Zacharia Vang'ota wa
kata changarawe,Chesco lyuvale wa Kata ya kinyanambo walimtaka
Mwenyekiti wa halmashauri hiyo kuzisimamia ipasavyo sheria ambazo
zimetungwa na halmashauri pamoja na serikali ya jamhuli ya muungano wa
Tanzania chini ya Rais Dr John pombe Magufuli ili kukuza mapato katika
halmashauri hiyo.
"Ukiangalia
hapa Mafinga tunavyanzo vingi vya mapato lakini watalaamu wetu
hawavifanyii kazi ndio maana sisi madiwani tumeamua kuanzia sasa vyanzo
vyote tulivyovibainisha leo kwenye baraza vifanyiwe kazi haraka sana ili
kukuza mapato ya halmashauri yetu"walisema madiwani
Kwa
upande wao baadhi ya wananchi wa Mafinga Mjini walisema kuwa Mji huo una
changamoto nyingi hivyo serikali ya mji inatakiwa kuanza kuzitumia hizo
sheria Mpya haraka ili hata wananchi wayatambue maeneo yanayopaswa
kulipa kodi na kuewezesha halmashauri kukuza mapato na kutatua
changamoto za Mji wa Mafinga.
"Angalieni
nyie waandishi Mafinga maji ni tatizo kubwa,Barbara bado
hazijatengenezwa hasa huku mitaani kwetu,Mji bado mchafu kila mtu
anatupa takataka anavyotaka kwa kuwa hakuna mtu wa kumkamata ila
ukiangalia sheria Mpya zipo lakini hazifanyiwi kazi na Mafinga maeneo ya
maegesho ya magari hayalipiwi wakati miji mingine ni moja vya mapato
hivyo viongozi wanapaswa kuanza kuzitumia sheria Mpya" walisema wananchi
SHARE
No comments:
Post a Comment