TRA

TRA

Sunday, July 16, 2017

NDEGE ILIYOWAPELEKA MAJERUHI WA LUCKY VICENT MAREKANI KUWAREJESHA NCHINI

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !
Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu amesema kuwa ngege aina ya DC 8 itawarudisha Tanzania watoto Doreen, Saidia na Wilson mwezi ujao kama ilivyoondoka nao nchini.
Mhe. Nyarandu ametumia kurasa zake za mitandao ya kijamii kutoa taarifa hizo huku akisema kuwa wameshakubaliana na ndege hiyo kama walivyoondoka nao nchini itawarejesha na vifaa kwaajili ya hospitali hapa Tanzania.
Breaking:-NDEGE aina ya DC 8 inayomilikwa na @samaritanspurse KUWARUDISHA #Tanzania watoto Doreen, Sadia, na Wilson mwezi ujao. TUMEKUBALIANA kuwa ndege hiyo iwarudishe nchini WATOTO kama walivyoondoka, na kurejea na VIFAA kwa ajili ya hospitali hapa #TanzaniaNITATOA ratiba kamili yenye tarehe na saa ya kuwasili (ETA) kwa watoto wetu uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro mara taratibu zitakapokamilika. Asanteni wote kwa kuendelea kuwakumbuka katika Sala na dua zenu.


Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger