MBUNGE wa jimbo la Kibaha Vijijini ,Hamoud Jumaa akikabidhi magari matatu ya wagonjwa (ambulance) ambayo yatasaidia kubeba wagonjwa katika jimbo la Kibaha Vijijini.
………………………………………………………………………….
Na Mwamvua Mwinyi ,Kibaha Vijijini
MBUNGE wa jimbo la
Kibaha Vijijini ,Hamoud Jumaa amekabidhi magari matatu ya wagonjwa
(ambulance )ambayo yatasaidia kupunguza adha ya usafiri kwa wagonjwa
hasa mahututi na warufaa.
Kati ya magari hayo
,mawili yametokana na nguvu zake na moja ni msaada kutoka kwa Rais John
Magufuli ikiwa ni kati ya magari ya wagonjwa 67 yaliyogawanywa katika
maeneo mbalimbali nchini .
Aidha mbunge huyo
,ameiomba wizara ya afya kukipandisha hadhi kituo cha afya cha Mlandizi
kuwa hospitali ya wilaya ombi ambalo waziri wa afya,jinsia ,wazee na
watoto Ummy Mwalimu amekubali ombi hilo .
Jumaa aliyasema hayo
,viwanja vya shule ya msingi Mtongani ,Mlandizi wakati Ummy Mwalimu
alipokwenda kukabidhi magari hayo kwa niaba yake kwa halmashauri na
mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Kibaha.
Alieleza ,ameamua kujikita kutatua kero zinazowakabili kwa kwenda sambamba na kauli mbiu yake ya SISI KWANZA SERIKALI BAADAE .
“Ninamshukuru waziri Ummy kwa dhati ya moyo wangu kwa jitihada zake za kupigania gari moja kuletwa Kibaha Vijijini ,”
“Ni bahati kwetu kwani
zilikuwa ambulance 67 ambapo 50 zilielekezwa mikoa ya kanda ya ziwa
ambako idadi ya vifo vya mama wajawazito ni kubwa hivyo zilibaki 17
hivyo moja wapo ndio hiyo imekuja kwetu ” alisema Jumaa .
Alibainisha kuwa ,magari hayo ni sehemu ya kupunguza tatizo la usafiri linalokabili vituo na zahanati jimboni hapo .
Alisema ,serikali iangalie uwezekano wa kuwaongezea magari ya wagonjwa katika maeneo ya mbali kama Kwala na Magindu .
Hata hivyo Jumaa
akizungumzia ombi la kituo cha afya Mlandizi kupandishwa hadhi ,alisema
anaendelea kufanya jitihada za kutimiza vigezo vinavyotakiwa kupandishwa
hadhi ikiwemo kujenga uzio .
Alimshukuru makamu wa
rais kwa harakati zake za kuhakikisha juhudi hizo zinazaa matunda kwa
kuwachangia mifuko ya saruji 500 ,waziri mkuu nae alichangia mifuko hiyo
150 .
Wadau wengine
wamechangia kokoto tani 7 kwa sh. mil. 9.1, mchanga mil. 2.4 tofali sh.
mil 8.4, nondo tani moja sh. mil. 3.6 na fedha zake mwenyewe na hadi
sasa zimeshatumia sh .milioni 50 .
Jumaa aliwaomba wadau wa afya na serikali kuendelea kumuunga mkono ili tatizo hilo libakie historia.
Alichukua fursa hiyo pia ,kukabidhi vitanda 25 na mashuka 50 vilivyotolewa na Rais katika majimbo mbalimbali nchini .
Katika vitanda hivyo 20 ni vya kawaida na vitanda vitano ni kwa ajili ya kujifungulia .
Akikabidhi magari hayo
ya wagonjwa ,waziri wa afya ,jinsia ,wazee na watototo Ummy alisema
atachangia mifuko ya saruji 100 ili kuunga mkono ujenzi wa uzio.
“Nampongeza Jumaa na mmepata mbunge anaejua kujiongeza ,mtumieni ,mtieni nguvu kwa mambo anayowapigania ” alisema Ummy .
Alisema kutoka na ahadi
walizowahi kutoa wakubwa wake kupandisha hadhi kituo hicho cha afya na
kwa kuwa ni wakubwa wake amekubali ombi hilo .
Ummy alisema pia kuna
fedha anaitegemea ambayo atawezesha kujenga wodi ya uzazi yenye sehemu
mbili na maabara ya damu kwa lengo la kuboresha huduma za afya .
“Vigezo vikikamilika
kwa namna hiii ,idadi ya watu wanaohudumiwa ,uzio ,idadi ya majengo na
mengineyo naamini tutapata hospital ya wilaya iliyo nzuri na
iliyokamilika ” alifafanua Ummy .
Mwenyekiti wa
halmashauri ya wilaya ya Kibaha ,Mansoor Kisebengo ,alisema
watahakikisha wananchi hawagharamii mafuta kwa magari hayo .
Kisebengo alisema ,halmashauri hiyo itakuwa inachangia gharama za mahitaji ya mafuta ili kuondoa bugudha kwa wananchi .
SHARE
No comments:
Post a Comment