Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuzindua barabara ya
Manyoni-Itigi-Chaya yenye urefu wa Kilomita 89.3 mapema jana, kulia kwake
ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Makame Mbarawa na kushoto
kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wakazi wa Itigi mara
baada ya kuzungumza nao na kuzindua barabara Manyoni-Itigi-Chaya,
ambapo pamoja na mambo mengine ameagiza ujenzi wa barabara ya
Chaya-Nyaua yenye kilomita 85 na ujenzi uanze ndani ya siku 45 ili
barabara hiyo ikamilike kwa kiwango cha lami.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na umati wa wakazi wa
Itigi waliojitokeza kumlaki na kushuhudia uzinduzi wa barabara ya
Manyoni-Itigi-Chaya, Rais Magufuli amewataka wana Itigi kutumia fursa ya
kuwa jirani na Makao makuu ya nchi kwa kufanya kazi kwa bidii na
kuzalisha bidhaa ambazo zitauzwa huko Dodoma.
Umati wa wakazi wa Itigi
waliojitokeza kumlaki Rais Magufuli na kushuhudia uzinduzi wa barabara
ya Manyoni-Itigi-Chaya, wakazi hao wamempongeza na kumshukuru Rais
Magufuli kwa kuwajengea barabara hiyo ambayo ni muhimu kwa kuwaunganisha
na mikoa ya Tabora na Kigoma.
Sehemu ya barabara ya
Manyoni-Itigi-Chaya ambayo imezinduliwa leo na Rais Magufuli, Barabara
hiyo yenye urefu wa kilomita 89.3 kwa kiwango cha lami imefungua fursa
ya usafirishaji kwa urahisi kutoka kanda ya Kati yaani Singida na Dodoma
Kuelekea mikoa ya Tabora na Kigoma hadi nchi za jirani za Burundi na
Kongo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Makame Mbarawa akimkaribisha Rais Magufuli azungumze na
wananchi wa Itigi, ambapo amesema barabara ya Manyoni Itigi Chaya
imegharimu shilingi bilioni 114.692 na kiunganishi cha Mikoa ya Singida,
Tabora na Kigoma kuelekea Makao makuu ya Nchi yaani Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema
Nchimbi akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili eneo la Njiapanda Itigi,
alipozungumza na wananchi wa eneo hilo na kuzindua barabara ya
Manyoni-Itigi-Chaya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiambatana na Mkuu wa Mkoa wa Singida
Dkt Rehema Nchimbi kwenye eneo la mkutano wa hadhara mara baada ya
kuwasili eneo la Njiapanda Itigi, alipozungumza na wananchi wa eneo hilo
na kuzindua barabara ya Manyoni-Itigi-Chaya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amkimsikiliza kwa makini Mhandisi wa
TANROADS mkoa wa Singida Leonard Kapongo mapema jana. Katika mkutano wa
hadhara na wananchi wa Itigi, Rais Magufuli amemuagiza Meneja huyo na
Wizara ya ujenzi kupitia upya gharama za ujenzi wa barabara ya Itigi
Makongorosi yenye urefu wa kilomita 57 ambapo gharama za ujenzi wa
barabara hiyo ni bilioni 104.
SHARE
No comments:
Post a Comment