Mkurugenzi mpya wa michezo wa klabu ya AS Roma, ameitahadharisha
Manchester United isipoteze muda wake kuhusu mpango wake wa kumsajili
mchezaji wao, Radja Nainggolan kwani haendi popote katika msimu huu wa
kiangazi. Raia huyo wa Ubelgiji amekuwa akihusishwa kwa kiasi kikubwa
kujiunga na Mashetani Wekundu, pia mwaka jana klabu ya Chelsea
ilikaribia kumsajili lakini mpango huo ukayeyuka.
Mchezaji
huyo mwenye miaka 29 ameimarika kuwa miongoni mwa viungo tishio duniani,
hivyo uongozi wa klabu hiyo ya Italia imetangaza rasmi haitamuachia
kwenda klabu yoyote msimu huu wa kiangazi.
SHARE
No comments:
Post a Comment