Shabiki wa soka, Vivien Bodycote, 59, ameamua moyo wake ufanye kazi
mbili kwa wakati mmoja, kwanza ni kusukuma damu, pili ni kuhifadhi
upendo wake kwa Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho.
Inawezekana
hilo likawashangaza wengi lakini ukweli ndiyo huo kuwa Vivien ni
shabiki mkubwa wa kocha huyo raia wa Ureno ambaye pia ni baba wa watoto
wawili.
Vivien
hajaficha hisia zake, bali ameziweka wazi kiasi kwamba hata mumewe, Tony
ambaye ana umri wa miaka 76, anafahamu jinsi mkewe anavyomkubali kocha
huyo na ndiyo maana wawili hao wametumia zaidi ya pauni 800 (Sh milioni
2.3) kuchora tatuu zenye taswira au zinazohusiana na kocha
huyo.Akielezea zaidi, Vivien anasema: “Huwa ni nadra kwangu kwenda mjini
kisha nirejee nikiwa sina tatuu ya Jose mwilini mwangu, nina tatuu 20
zinazomhusu yeye. Siyo kwamba ni mtu muhimu, ni mtu wa kipekee
kwangu.“Nitafurahi sana nikikutana naye, nipo tayari hata kumsaliti mume
wangu linapokuja suala la Mourinho. Ni mtu mwenye mwonekano wa tofauti,
kila mara ninapofunua gazeti na kumuona huwa napata washawasha kwenye
magoti.
“Bei za
tatuu zangu zipo tofauti, kuna ambazo nilichora kwa gharama ndogo ya
pauni 60 (Sh 171,850) lakini nyingi ni za pauni 250 (Sh 716,040). Kwa
jumla zimenigharimu kama pauni 800.”
Vivien
ambaye ni mkazi wa mtaa wa Hinckley Kitongoji cha Leicestershire
hajawahi kwenda uwanjani tangu alipofanya hivyo miaka ya 1900, alipoenda
akiwa na baba yake ambaye kwa sasa ni marehemu lakini hiyo haijamzuia
kuwa shabiki mkubwa wa soka.
Shabiki
huyo ambaye umri umemtupa mkono ni bibi mwenye wajukuu, alifunga ndoa na
mume wake wa sasa miaka 15 iliyopita, ameongeza: “Hakuna siku ambayo
inapita bila mimi kuitazama picha ya Jose mtandaoni, nimeathirika kwa
Jose Mourinho.
“Nimekuwa
nikiulizwa na majirani kuwa kwa nini nisiwe shabiki wa Leicester lakini
mimi ambacho ninawajibu ni kuwa nipo kwenye penzi zito na kocha huyo wa
soka.
“Kama
akiamua kuondoka Manchester United kwenda nje ya nchi kufundisha hata
mimi pia nitaacha kushabikia soka la Uingereza, nitamfuata huko
atakapokwenda.
“Mjukuu
wangu aliponiambia wakati Jose alipofukuzwa Chelsea, nilifuta sherehe
zote za Krisimasi na hakukuwa na mlo wa usiku kipindi hicho, nilitamani
kukutana naye na nimweleze hisia zangu jinsi nilivyoumia, nimpoze.”
Ajabu ni
kuwe, mume wa Vivien ndiye ambaye amekuwa akitoa fedha ili mkewe
akajichore tatuu hizo za Mourinho kutimiza furaha yake.
Akizungumzia
hali hiyo, Tony anasema: “Anafanya anachopenda huwa sijali kuhusu
kumuongezea fedha au kumpa fedha za kujichora tatuu, najua zina gharama
kubwa lakini sijui gharama yake halisi.
“Sijawahi
kupenda mpira na wala siyo shabiki wa mchezo huo lakini miaka michache
iliyopita ndipo nilipoanza kufuatilia kidogo japokuwa sikuwahi kwenda
uwanjani, lakini yeye (mkewe) anapenda.”
Upande wa
bibi mwenyewe anasisitiza kwa kusema: “Nimekuwa sifikirii idadi ya
tatuu nilizonazo kwa kuwa kila ninapomaliza kuchora moja huwa nafikiria
nyingine. Tony huwa ananipeleka sehemu za kuchorea na kuniacha.”
Kuna
tatuu ambayo ameiandika Mrs Mourinho akimaanisha yeye ndiye mke wa
Mourinho kisha pembeni yake kuna tatuu ya sura ya Mreno huyo.
SHARE
No comments:
Post a Comment