TRA

TRA

Tuesday, July 25, 2017

Marekani kuipa Ukraine silaha za kupambana na waasi

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !
Mjumbe mpya wa Marekani nchini Ukraine anasema kuwa Marekani inatathmini ikiwa itatuma silaha kusaidia wale wanaopigana na waasi wanoungwa mkono na Urusi.

Kurt Volker aliiambia BBC kuwa kuihami serikali ya Ukrain itabadilisha msimamo wa Urusi. Alisema hafikirii kuwa hatua hiyo itakuwa ni uchokozi.
 Rais wa Ukraine Petro Poroshenko (wa pili kulia) akikutana na  maofisa huko Donetsk mwezi Juni
Wiki iliyopita wizara ya mashauri ya nchi za kigeni ya Marekani ilizitaka pande zote mbili kusitisha mapigano mashariki mwa Ukraine.

"Silaha za kujilinda, zile ambazo zitaisaidia ukrain kujilinda na kuharibu vifaru kwa mafano, ambazo zitaizuia Urusi kuitisha Ukrain," bwana Volker aliiambia BBC. 

Alisema kuwa mafanikio ya kuwepo amani mashariki mwa Ukrain yanahitaji kile alichokitaja mchakato wa mazungumzo na Urusi.
Bwana Volker na mjumbe wa zamani wa Marekani kwenye Nato na aliteuliwa kwenye wadhifa huo mpya mwezi huu.
Umoja wa Mataifa unasema kuwa zaidi ya watu 10,000 wameuawa tangu mzozo wa Mashariki mwa Ukrain ushuke mwezi Aprili mwaka 2014 mara baada ya Urusi kulimega eneo la Crimea.
Mapigano hayo yamesababisha zaidi ya watu milioni 1.6 kuhama makwao.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger