Watu
wasiojulikana wanadaiwa kumuua kwa kumpiga risasi, mkazi wa Kijiji cha
Ruaruke, wilayani Kibiti, Mkoa wa Pwani Ramadhani Mzurui, usiku wa
kuamkia leo.
Kadhalika watu hao walimjeruhi mguuni kwa risasi mke wa marehemu.
Mganga
wa zamu katika Hospitali ya Mchukwi, Dk Emmanuel Humbi amethibitisha
kufikishwa hospitalini hapo kwa mwanamke huyo akiwa na majeraha ya
kupigwa risasi na kusema kwa sasa yupo katika chumba cha matibabu ya
dharura.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji, Onesmo Lyanga amesema tayari polisi
wamekwenda eneo la tukio kwa ajili ya uchunguzi wa tukio hilo.
SHARE
No comments:
Post a Comment