Rais
mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa ametembelea na kuzindua nyumba
ya wahudumu wa afya katika kijiji cha Mkungo wilayani Chato mkoani
Geita zilizojengwa na taasisi ya Mkapa Foundation kwa kushirikiana na
Serikali.
Akizindua
nyumba hizo jana, Rais Mkapa aliwasalimia wanachi kwa salam yake ya
“mambo” na wananchi kuitika poa” na kuwataka kutunza nyumba hizo na
kushirikiana vema na watumishi watakaoshi katika nyumba hizo kisha
msafara wake kuondoka na kuelekea Ikulu ndogo iliyopo Chato.
Mkapa
aliingia katika eneo la zahanati hiyo saa sita mchana akiongozana na
mkewe, Mama Anna Mkapa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu.
Uzinduzi wa nyumba hiyo ni ishara ya kuzindua nyumba nyingine 50 zilizopo katika mikoa ya Geita, Simuyu na Kagera .
Makabidhiano
ya nyumba hizo yanatarajiwa kufanyika leo (Jumatatu Julai 10) katika
uwanja wa mpira wa miguu uliopo Chato mjini hafla itakayohudhuriwa na
Rais John Magufuli.
Ofisa
Uhusiano na Mawasiliano wa Mkapa Foundation, Deogratius Rimoy alisema
nyumba 50 zilizojengwa na taasisi hiyo katika mikoa mitatu tofauti
zimegharimu kiasi cha Sh 2.5 bilion
Alisema
lengo la kujenga nyumba hizo ni ili kuboresha huduma za afya vijijini
illi watumishi waweze kutoa huduma za afya kwa saa 24.
SHARE
No comments:
Post a Comment