TRA

TRA

Monday, July 10, 2017

WAZIRI WA KENYA ATANGAZA AMRI YA KUTOTEMBEA USIKU

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !
 
Kaimu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya, Fred Matiangi, ametangaza amri ya kutotembea usiku kwa miezi mitatu katika County za Lamu, Tana River na Garissa ambazo zimekuwa zikishambuliwa mara kwa mara na wanamgambo wa Al – Shaabab.
Amri hiyo imetangazwa baada ya Bw. Matiangi kukutana na Rais Uhuru Kenyatta wakati wa kikao cha Baraza la Taifa la Usalama la nchi hiyo.

Amri hiyo itaanza kutekelezwa mara moja kuanzia saa 12:30 jioni hadi saa 12:30 asubuhi katika County hizo tatu na maeneo ya jirani ambayo yanaonekana kuwa hatari.

Hata hivyo, Matiangi, amesema amri hiyo haitahusu visiwa vya Lamu, Manda na Pate.

Ijumaa ya wiki jana usiku, watu tisa waliuwawa kwa kuchinjwa na wanamgambo wa Al – Shaabab katika vijiji vya Jima na Poromoko katika County ya Lamu, ambapo siku ya Jumatano wanamgambo hao walivamia kituo cha polisi na kuwaua maafisa watatu.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger