Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Salum Hapi ameongea na wanahabari muda mfupi uliopita. Hii ni kutokana na mkutano mwingine na waandishi habari uliofanywa na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee hapo jana. Hapi ameongea yafuatayo:
- Jana Mbunge Halima Mdee ametoa kauli zinazolenga kumfedhesha Rais wetu na kuleta uchochezi.
- Halima Mdee anasema ipo siku Rais ataagiza wananchi watembee vifua wazi. Nimeshtushwa sana.
- Kwamba Mdee anasema Rais wetu ni wa ovyo, huu ni uchochezi na asingefaa kuyatoa kama kiongozi anayetakiwa awe na maadili.
- Kwa mamlaka niliyonayo naagiza Halima Mdee akamatwe na Jeshi la Polisi na awekwe ndani saa 48 na ahojiwe.
- Halima anasema Rais awekwe breki, nataka akawaambie Jeshi la Polisi hiyo breki ni ya aina gani.
- Nawataka wanasiasa wote katika wilaya yangu wasitoe kauli kama za Halima Mdee na sitowavumilia.
SHARE
No comments:
Post a Comment