AFRIKA Kusini
MOTO mkubwa umewaka katika jengo la ghorofa na kusababisha taharuki kubwa, huku mamia ya watu wakihofiwa kupoteza maisha.
Kutokana na tukio hilo wengine waliamua kufunga kamba dirishani ili kuondoka katika jengo hilo wakati moto ukiendelea kuwaka.
Wafanyakazi wa kitengo cha dharura walikaririwa wakisema kuna uwezekano watu wengi wamepoteza maisha katika tukio hilo ambalo limetokea leo Jumatano.
Tayari watu 50 wameokolewa na wengine wanaendelea kupatiwa matibabu, alisema msemaji wa kituo hicho, Nana Hadebe na kubainisha kuwa moto huo tayari umezimwa na chanzo chake hakijafahamika.
SHARE
No comments:
Post a Comment