Watoto
watano waliofanyiwa upasuaji na kuwekewa vifaa maalum vya kusaidia
kusikia (Cochlear Implant) jana wamewashiwa vifaa hivyo ili waweze
kusikia kwa mara ya kwanza. Zoezi hilo limefanywa na wataalam wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kushirikiana na watalaam kutoka MEDEL .
Daktari
Bingwa wa magonjwa ya Masikio, Pua na Koo Edwin Liyombo amesema Juni
5 na 6 mwaka huu watoto hao walifanyiwa upasuaji huo kwa mara ya kwanza
na kuwekewa vifaa maalum kwa ajili ya kusikia (Internal complete)
lakini leo wamekuja kuwekewa na kuwashiwa vifaa vya nje(External
complete) ili waweze kusikia.
Kwa
upande wake mtaalam wa vifaa vya usikivu Fayaz Jaffer amesema baada ya
kuwekewa kifaa hivyo watoto hao wanapaswa kurudi kila baada ya wiki
mbili kwa miezi mitatu na baada ya hapo watarudi wiki mbili kwa miezi
sita ili kufanyiwa mazoezi.
‘’Baada
ya hapo wanaanza kuwafanyia mazoezi ya kuongea ( speech therapy) ndani
ya mwaka mmoja na kadiri umri unavyozidi kwenda watakuwa wameshaanza
kusikia na kujifunza kuongea na kupelekwa kujifunza zaidi katika shule
za kawaida na si shule maalum kama ilivyozoeleka” amesema mtaalam huyo.
Juni
7 mwaka huu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto
Ummy Mwalimu alizindua huduma ya upasuaji wa kupandikizaji wa vifaa vya
usikivu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili , ambapo katika Hospitali
za Umma Tanzania imekuwa nchi ya kwanza kutoa huduma hiyo na ya pili
katika nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki ikitanguliwa na Kenya.
Mwakilishi
wa Medel Afrika Mohamed El Disouky akimfanyia mazoezi ya kuzungumza
mtoto Asma Athuman Mwinyi ambaye alipata matatizo ya kusikia akiwa na
miaka sita.
Mtaalam
Mohamed El Disouky akimfanyia majaribio ya kifaa cha usikivu mtoto
Silas Machaku ( 3 ) ambaye aliwekewa kifaa maalum cha usikivu kwa ndani
(Internal complete) lakini leo amewekewa kifaa kwa nje (External
complete) ili aweze kusikia . zoezi hilo limefanyika katika Hospitali ya
Taifa Muhimbili.
SHARE
No comments:
Post a Comment