Msanii
wa Bongo, Lady Jaydee amempa pongezi za kutosha msanii mwenzie
Professor Jay kwa uamuzi aliyofikia wa kufunga ndoa.Weekend iliyopita
siku ya Jumamosi Prof Jay alifunga ndoa na mchumba wake wa siku nyingi
‘Grace’ ambaye tayari walishajaliwa mtoto mmoja.
Kuhusu
hilo Lady Jaydee amesema, “Kwanza nimpongeze Prof Jay kwa hatua
aliyochukua, ni hatua nzuri katika maisha kwa sababu kwanza ni kuzaliwa,
pili ni kuoa au kuolewa na ya tatu ni kufa, kwa hiyo hii ni harusi ya
pili katika maisha yake nimpongeze sana kwa uamuzi alioufikia,”
ameiambia Planet Bongo ya EA Radio na kuongeza.“Nimtakie kila la kheri
katika maisha yake ya ndoa yenye furaha na mafanikio. Professor kama
kaka yangu na kama rafiki yangu ni mambo mengi tumepitia pamoja,
tumeweza kusapotiana katika kazi na mambo mengine, kwa hiyo ni furaha
kwangu, si kama msanii mwenzake bali kama mwanafamilia,” ameeleza Lady
Jaydee.
Professor
Jay na Lady Jaydee wamesharikiana katika nyimbo nyingi kama vile Kikao
cha Dharura, Bongo Dar es Salaam, Niamini na Joto Hasira.
SHARE
No comments:
Post a Comment