Mkurugenzi, Idara ya Ushirikiano
wa Kikanda toka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Balozi Innocent Shiyo akizungumza na waandishi wa habari (hawapo
pichani) kuhusu mazungumzo ya pamoja kuhusu mahusiano ya kibiashara kati
ya Serikali ya Tanzania na Kenya mapema hii leo jijini Dar es Salaam,
kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania
Balozi Dkt. Augustine Mahiga.
Baadhi ya waandishi wa habari
wakimfuatilia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa
Tanzania Balozi Dkt. Augustine Mahiga (hayupo pichani) wakati akitoa
ufafanuzi kuhusu mazungumzo ya pamoja kuhusu mahusiano ya kibiashara
kati ya Serikali ya Tanzania na Kenya mapema hii leo jijini Dar es
Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania Balozi Dkt. Augustine Mahiga
(kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu
mazungumzo ya pamoja kuhusu mahusiano ya kibiashara kati ya Serikali ya
Tanzania na Kenya mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni
Mkurugenzi, Idara ya Ushirikiano wa Kikanda toka Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Innocent Shiyo na kushoto ni Kaimu
Balozi wa Kenya nchini Tanzania Peter Sang.
Picha na Eliphace Marwa -Maelezo
…………………………..
Na: Paschal Dotto – MAELEZO
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Serikali ya Kenya zimefanya mazungumzo ya pamoja na kutatua
vikwazo vilivyokuwa vikiikabili sekta ya biashara baina ya nchi hizo.
Akizungumza na waandishi wa habari
leo, Jijini Dar es Salaam Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga ametoa taarifa juu ya
kumalizika kwa tofauti za kibiashara baina ya nchi hizo.
“Bidhaa za Tanzania zilizowekewa
vikwazo na nchi ya Kenya ni unga wa ngano pamoja na gesi ya kupikia
(LPG). Aidha juhudi, za Serikali ya Tanzania kuona vikwazo hivyo
vinaondolewa na Serikali ya Kenya kwa wakati hazikuzaa matunda, hivyo
Serikali ya Tanzania nayo iliweka vikwazo kwa bidhaa za maziwa na sigara
kutoka Kenya kuingia katika soko la Tanzania,” amefafanua Dkt. Mahiga.
Amesema kuwa kutokana na mahusiano
mazuri ya udugu yaliyopo kati ya Tanzania na Kenya na kwa kujali
manufaa mapana ya Jumuiya ya Afrika Mashariki viongozi wakuu wa nchi
hizo mbili, Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
walikubaliana kuzungumza na kutoa vikwazo vya biashara hizo.
Aidha, Dkt. Mahiga amesema, nchi
hizo zimekubaliana kuunda Tume ya pamoja ambayo itakuwa na jukumu la
kuepusha tofauti za kibiashara kati ya Tanzania na Kenya pamoja na
kutolea ufumbuzi changamoto za kibiashara kati ya nchi hizo mbili pindi
zinapojitokeza.
Tume hiyo itaongozwa na Mawaziri
wa mambo ya Nje wa Tanzania na Kenya na kujumuisha mawaziri wanaohusika
na masuala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Biashara, Fedha, Mambo ya
Ndani ya Nchi, Kilimo, Uchukuzi na Utalii wa nchi hizo.
SHARE
No comments:
Post a Comment