Mwandishi Wetu, Mbeya
WAENDESHAJI wa bahati nasibu ya Biko, ‘Ijue Nguvu ya Buku’, jana wamemkabidhi Sh. milioni 20 mshindi wao wa droo ya 18, Linda Mhewa, ambaye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) kilichopo jijini Mbeya.
Mwanafunzi huyo ambaye ni msichana wa pili kufanikiwa kuzoa mamilioni ya Biko kupitia bahati nasibu ya Biko, aling’ara katika droo ya Jumatano iliyopita, ikiwa ni mwendelezo wa bahati nasibu hiyo kumwaga mamilioni kwa kupitia mchezo wao unaotoa zawadi za papo kwa hapo kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh.
Milioni moja, bila kusahau droo kubwa ya Jumatano na Jumapili ya Sh Milioni 20. Akizungumza katika makabidhiano hayo, Mhewa aliyetangazwa kuwa mshindi wa donge nono la Sh. Milioni 20, alisema kwamba ni furaha yake kuona Mungu amemchagua katika bahati nasibu hiyo inayotikisa hapa nchini tangu kuanzishwa kwake.
Alisema amekuwa mchezaji mzuri wa Biko, huku akiamini kuwa kushinda kwake ni sehemu ya kubadilisha maisha yake kiuchumi jambo ambalo ndilo alilokusudia kiasi cha kuamua kucheza Biko.
"Wakati napigiwa simu na Kajala sijaamini kabisa, nikaamini baada ya kuona ni kweli hususan baada ya kukabidhiwa fedha zangu ikiwa ni matokeo ya kucheza kwangu Biko, huku ukiwa mchezo rahisi kwa sababu kwa kutumia simu za mikononi za Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money kwa kuingiza namba ya kampuni 505050 na ile ya kumbukumbu 2456, huku kianzio cha kucheza kikianzia Sh 1,000 na kuendelea,” alisema Mhewa.
Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven alimpongeza mshindi wao wa jijini Mbeya, huku akimtaka ahakikishe kuwa uchumi wake unakua kwa kuhakikisha kwamba anazitumia vyema fedha alizoshinda kutoka kwenye bahati nasibu yao.
''Ni jambo zuri kuinuka kiuchumi kwa kupitia mchezo huu wa kubahatisha wa Biko, ambapo tumeshuhudia mamia ya Watanzania wakiibuka kidedea katika droo za wiki pamoja na ushindi wa papo kwa hapo unaotoka kila dakika,'' alisema.
Kwa mwezi Mei pekee, zaidi ya Sh. Milioni 500 zimetolewa kwa washindi, huku donge nono la Sh Milioni 20 likienda kwa washindi wawili kwa droo ya Jumatano na Jumapili.
Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven (kulia) akiwa katika moja ya majukumu.
SHARE
No comments:
Post a Comment