Mwandishi Wetu
Mfuko wa Pensheni wa LAPF umeendelea na shughuli zake za kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi wanaotembelea banda lao lililopo katika Maonesho ya Biashara maarufu kama Sabasaba.
Kwa mujibu wa Ofisa Masoko Mwandamizi wa mfuko huo, Rehema Mkamba watatumia maonesho hayo kuhakikisha wanahudumia wananchi wengi zaidi na kuandikisha wanachama wa hiari ili waendelee kunufaika na huduma za LAPF.
Ukijiunga na LAPF hutajutia kamwe kwa sababu unaweza kupata mikopo ya nyumba, mkopo kwa ajili ya SACCOS, mkopo wa elimu,mkopo wa kujikimu na mengine mengi ya aina hiyo. Muhimu ni kuwahi kwenye banda lao ili unufaike na huduma za mfuko huo.
Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa LAPF Bw. James Mlowe akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea katika banda la mfuko huo kwenye maonyesho ya Biashara ya Kimataifa yanayoandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) yanayofanyika kwenye viwanja vya Sabasaba Barabara ya Kirwa jijini Dar es salaam.
SHARE
No comments:
Post a Comment