Bi
Santos amechukua udhibiti wa benki hiyo ya BFA baada ya kampuni yake
kununua hisa zaidi katika benki hiyo na kudhibiti zaidi ya asilimia 50
ya hisa katika benki hiyo.
Hatua hiyo imewaacha waangalizi kutojua ikiwa
watamshangilia mama huyu mjasiria mali au kulalamikia mamlaka na
ushawishi wa kiuchumi walio nao matajiri wachache sana barani Afrika.
Isabel dos Santos mwenye umri wa miaka 43, amefanikiwa na angali
na ari ya kufanikiwa zaidi katika kanda ambayo wanaume wanatawala katika
ofisi nyingi za umma na za kibinafsi.Bi Dos Santos, ni bintiye rais wa
angola Jose Eduardo dos Santos, ambaye ameongoza taifa hilo tangu mwaka
wa elfu moja mia kenda na sabini na tisa.
Angola ni moja ya mataifa
masikini zaidi duniani.
Katika
miaka ya hivi karibuni ilinufaika pakubwa kutokana na mapato
yanayotokana na mauzo ya mafuta na uwekezaji kutoka uchina.
Hata hivyo, ufisadi na umaskini vimesalia kuwa changamoto kubwa zaidi nchini humo. Bi
Dos Santos mara kwa mara amepuuzilia mbali madai kuwa familia ya rais
inapewa nafasi zaidi kuliko raia wengine kuthibiti uchumi na masuala ya
kisiasa ili kuhakikisha kuwa familia hiyo itaendelea kutawala Angola
baada ya rais Dos Santos kustaafu, kama alivyohaidi hivi majuzi.Kwa sasa
Bi Dos Santos anasimamia shirika la mafuta la taifa na kampuni kubwa
zaidi ya kutoa huduma za simu na sasa anadhibiti benki kubwa zaidi
nchini Angola BFA.
Hii
ikiashiria kuwa ushawishi wa familia ya rais dos santos itaendelea
kuchukua nafasi kubwa zaidi katika masuala ya kiuchumi na kisiasa nchini
Angola miaka zijazo.
SHARE
No comments:
Post a Comment