Tiganya Vincent
RS-TABORA
Katibu
Tawala Mkoa wa Tabora, Dk. Thea Ntara amemtaka Mganga Mfawidhi wa
Hospitali ya Rufaa ya Kitete kuwakamata mara moja na kuwafikisha Polisi
watumishi wawili wa hospitali hiyo wanaotuhumiwa kukutwa na dawa na
vifaa tiba katika mikoba yao.
Dk.
Ntara alitoa kauli hiyo jana mjini Tabora baada ya watumishi hao
kukamatwa na vifaa hivyo katika mikoba yao kinyume na utaratibu wa
hospitali na ambazo dawa hizo na vifaa wanatuhumiwa walikuwa wakitaka
kwenda kuziuza katika hospitali binafsi.
Alisema
kuwa baada ya kukamatwa na kupekuliwa katika mikoba yao ndipo walikuwa
na dawa na vifaa tiba ambavyo havitakiwa kutoka nje ya hospitali na
havikuwa na maelekezo ya Mganga.
Kutokana na kazi hiyo ilifanywa na walinzi hao Katibu Tawala huyo wa Mkoa
aliwapongeza na kuwaagiza kuongeza kupekua watu wote wanaokwenda kuona
wagonjwa kwa sababu yawezekana watumishi wengine ambao sio waadilifu
wakatumia nafasi hiyo kutorosha dawa na vifaa tiba.
Alimwagiza
Mganga Mfawaidhi wa Hospitali hiyo kuhakikisha watuhumiwa hao
wanakamatwa mara moja na kufikishwa Polisi wakati hatua nyingine za
kiutumishi zinaendelea.
Watumishi
waliokamatwa kwa tuhuma za kukutwa na dawa na vifaa tiba katika mikoba
yao ni Petronila Mbipa Bundala ambaye ni Mhudumu na Monica Alexanda
Rugeinamu ambaye ni Muuguzi.
Aidha
ameagiza watumishi hao waandikiwe mara moja barua za kusimamishwa kazi
kutokana na tuhuma za kukutwa na mali ya mwajiri wao kinyume na sheria.
Vifaa na dawa vilivyokamatwa ni Cannula, Surgical gloves, Syringesa, Urinal bag, IV giving set, Blood giving set,
Brainded silk number, water injection, powder, soap, examination grolve, gentamyacin injection ampule, ascorbic acid.
Hivi
karibuni Hospitali hiyo imekumbana na wizi wa mara kwa mara hatua
iliyopelekea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora kusimamisha kampuni
iliyokuwa imepewa jukumu la kulinda na kulazimika kuweka Kampuni
nyingine wakati taratibu za kuichukulia hatua Kampuni ya awali
zikiendelea.
SHARE
No comments:
Post a Comment