Rais
mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete amesema kuwa ipo haja ya kuzalisha
wataalamu zaidi ili kukwepa kupeleka wagonjwa nje ya nchi.
Amesema
hayo jana Jumatatu, Julai 24, alipokuwa akizindua mkutano wa siku mbili
uliozikutanisha nchi 12 zikiwamo za Afrika ili kujadili utoaji wa
huduma za afya hususani katika sekta binafsi.
Alisema
katika majukwaa ni rahisi kusema hakuna haja ya kupeleka wagonjwa nje
ya nchi kwa ajili ya kupata matibabu, lakini kiuhalisia jambo hilo
haliwezekani kwa sababu wataalamu waliopo ni wachache.
Alitolea
mfano nchi nzima kuna wataalamu watatu wa upasuaji wenye utaalamu wa
mishipa ya fahamu ambao hawatoshi ukilinganisha na idadi ya Watanzania
wanaofikia 50 milioni.
Rais
Kikwete pia alitumia mkutano huo kuwaasa wahudumu wa afya wa sekta
binafsi kusisistiza matumizi ya bima ya afya kwa wananchi badala ya
kung'ang'ania kudhaminiwa na Serikali kupata mikopo.
Alisema rais huyo mstaafu:
"Msijisumbue kwa hili Serikali haiwezi kuwadhamini wala msijidanganye,
haiwezi kufanya hivyo kwa sababu italazimika kutumia kodi za wananchi
kulipa mikopo iliyowashinda kulipa.
“Wananchi
wakiwa na bima ya afya mnaweza kujipanua hadi mikoani na mkafanya kazi
na kuacha kufanya mijini pekee ambako wananchi angalau wanaweza kumudu
gharama za matibabu," alisema.
Naye
Mkurugenzi wa Mfuko wa Mikopo-Afrika Mashariki Evelyne Gitonga alisema
asilimia 84 ya vituo vya afya binafsi nchini Tanzania havifanyi vizuri
kutokana na kukosa ruzuku kutoka serikalini na kutofikiwa na mikopo.
Alisema
kukosekana mikopo na fedha za kujiendesha husababisha kutoa huduma
chini ya kiwango hali inayosababisha wanaovitegemea kuendelea kuteseka.
Akizungumza
katika mkutano huo, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu alisema kuwa wataalamu
wanazalishwa kwa wingi changamoto iliyopo ni ajira.
Alisema
wanalifanyia kazi suala hilo ili kuhakikisha wanakuwa na rasilimali
watu ya kutosha ili kufanikisha azma ya utoaji huduma bora ya afya.
SHARE
No comments:
Post a Comment