Waziri
wa Afya, Ummy Mwalimu amewataka waganga wakuu wa mikoa na wilaya
kutowawekea vikwazo wataalamu wa tiba asili na mbadala ili waweze
kujisajili na kutambulika kisheria.
Mwalimu
ameyasama hayo jana Jumatatu Julai 24 wakati akizindua Mpango Mkakati
wa Tiba Asilia na Tiba Mbadala utakaoanza kutumika mwaka 2017 hadi mwaka
2022.
Alisema
si lengo la Serikali kukandamiza au kuzuia tiba asilia bali inataka
kuhakikisha dawa zinazotumika ni salama kwa afya za watumiaji.
“Ili
kujua kama dawa ni salama lazima wajisajili, dawa zao ziangaliwe na
inapothibitika kuwa ni salama basi zitumike, tusiwawakee vikwazo, ni
wajibu wetu kuwawekea mazingira wezeshi kufikia hatua hiyo,” alisema.
Alisema
zaidi ya asilimia 60 ya Watanzania wanatumia tiba mbadala na asilia
hivyo ni muhimu kuwepo uangalizi wa kutosha kuhakikisha dawa hizo
hazileti madhara kwenye jamii.
Mwenyekiti
wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala, Dk Edmund Kayombo alisema
watalaamu 16,200 pekee ndio wamesajiliwa kisheria kutoa tiba hizo.
“Tunawahamasisha
waje kujisajili, wapo wanaojitokeza ila wengi wao wanakwepa kwasababu
hawataki kuonyesha miti wanayotumia,”alisema.
SHARE
No comments:
Post a Comment