TRA

TRA

Friday, July 7, 2017

Rais wa klabu ajiuzulu kwa vitisho vya mashabiki Brazil

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


Rais wa klabu moja ya soka ya ligi ya daraja la pili nchini Brazil Paysandu Sport amejiuzulu akisema kuwa watu waliojihami wamemtishia kumuua iwapo klabu hiyo itashushwa daraja.

Sergio Serra alisema kuwa alifuatwa akitembea na familia yake na watu waliokuwa katika pikipiki na kutishiwa. Paysandu ina makao yake huko Belem na ni miongoni mwa kilabu kubwa kaskazini mwa Brazil.

 Rais wa klabu ya Paysandu Sport ajiuzulu Brazil kutokana na  vitisho vya mashabiki

Klabu hiyo imekumbwa na wakati mgumu na iko katika nafasi ya 16 katika ligi ya Serie B ,ikiwa nafasi moja pekee kushushwa daraja.

Christina Serra, dadake Sergio aliripoti katika mitandao ya kijamii kwamba nduguye alikuwa ameenda kujivinjari na mkewe pamoja na watoto siku ya Jumapili.

Mmoja wao ambaye alikuwa ameziba uso wake na shati , alisema kuwa ''Najua unakoishi, Iwapo Paysandu itashushwa daraja hadi Serie C, nitakuua wewe na mkeo na mwanao''.

Ndugu yangu alishituka na akaamua kufanya maamuzi ya kujiuzulu.

Soka ya ya Brazil imekuwa na wakati mgumu kukabiliana na ghasia za mashabiki kwa miongo kadhaa na wachezaji pia wamekuwa wakipokea vitisho. 

Mwaka 2011, aliyekuwa beki wa kushoto Robert Carlos alisema kuwa amepokea vitisho vya simu na watu wamekuwa wakilifuata gari lake wakiwa katika pikipiki baada ya klabu yake ya soka Corinthians kubanduliwa katika kombe la Copa Libertadores.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger