Mapigano makali yamezuka katika mji mkuu wa Syria Damascus jana
Jumapili, baada ya waasi kupenya usiku katika maeneo ya mji huo
yanayodhibitiwa na serikali kupitia njia za chini ya ardhi. Ulikuwa
uvunjaji wa kustukiza wa usalama wa mji huo mkuu, ambako serikali
imefanikiwa kuyazuwia majeshi ya waasi yaliopiga kambi katika maeneo
mawili katika upande wa mashariki wa mji huo. Wakaazi walisema makombora
na roketi vilikuwa vikitua katikati kabisaa mwa mji, na ukurasa wa
Facebook unaoendeshwa na kundi la wanaharakati uliripoti juu ya
mashambulizi ya ndege za serikali katika maeneo yalikotokea mapigano.
Kundi hilo lilisema wanajeshi wa ziada waliwasili kwa upande wa serikali
pamoja na vifaru kuzuwia mashambulizi hayo mchana.
Monday, March 20, 2017
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment